Hii inakuja kufuatia ziara ya Raisi Barack Obama nchini Cuba, ziara ambayo imezua hisia tofauti kwa wanadiplomasia duniani. Raisi Obama anakuwa Raisi wa kwanza wa Marekani kutembelea Cuba kwani nchi hizo mbili zina mzozo wa kisiasa uliodumu kwa takribani miaka 80 sasa.
Raisi Obama alisema juhudi za Google ni moja kati ya mipango yao ya kupanua huduma za internet zaidi katika kisiwa hicho.
Google wametengeneza studio kubwa yenye simu nyingi za kisasa, Laptops (kompyuta pakato) pamoja na vifaa vingine vya kisasa katika jengo linalomilikiwa na msanii maarufu wa vinyago bwana Alexis Leiva Machado, maarufu kama Kcho.
Mkuu wa Google nchini Cuba bwana Brett Perlmutter, alisema ushirikiano wa Google na bwana Kcho ni mwanzo tu wa mpango mkubwa wa Google wa kusambaza huduma ya internet ya uhakika nchini humo.
Studio hiyo itakuwa wazi siku tano za wiki kuanzia saa moja asubuhi huku ikiwa na uwezo wa kupokea watu 40 kwa wakati mmoja.
Projecti hiyo inaonekana bado haijakubalika na baadhi ya wakuu wa idara za usalama nchini Cuba kwa kuhisi kurusu matumizi ya moja kwa moja ya mtandao yataathiri sana usalama ndani ya kisiwa hicho cha Kijamaa.