FUATA NJIA ZIFUATAZO KUREJESHA MAFAILI YALIYOPOTEA
1. Kwanza kabisa inabidi Kupakua (download) programu (Software) ya Asoftech
2. Baada ya kupakua (download) fanya mpango wa kuifadhi (install) itakuchukua muda kidogo tuu 3. Kutumia Asoftech inakubidi uwe ‘Administrator’ katika kompyuta yako, kama ni Admin nenda mpaka kwenye icon ya Asoftech ‘ Right Click’ kisha bofya ‘ Run As Administrator ‘.
4. Baada ya hapo unganisha simu yako au kifaa kingine katika kompyuta yako. Hakikisha kompyuta yako inasoma memori kadi ya simu yako. Au kama unaweza toa memori kadi ya simu weka katika sehemu ya kusoma kadi (card reader)na uunganishe katika kompyuta. Kama unataka fufua mafaili katika Hard Disk Drive ya kompyuta yako unaweza ruka hatua hii.
5. CHAGUA Diski Uhifadhi (DRIVE)
Chagua Drive Hatua ya hapo juu ikipita na Asoftech ikifunguka zitatoka orodha ya diski uhifadhi kibao, chagua moja ambayo unataka kufufua data zake. Chagua drive ya Sd card au Hard drive nyingine na kisha bofya NEXT
6. Itaanza fanya uchambuzi katika diski/ SD card yoyote uliyoichagua. Uchambuzi ukishakamilika itatoa orodha ya mafaili mengine na maelezo ya aina zake (kama vile mp3 au .jpg na zingine)
7. FUFUA MAFAILI
Fufua Mafaili Sasa unaweza kubonyeza “recover’ kufufua mafaili uliyo yachagua na pia unaweza kutochagua mafaili ambayo hutaki kuyafufua.
Kwa kutumia njia hii unaweza fufua aina yoyote ya faili katika Hard Disk Drive na hata SD card