Vifaa vya mawasiliano vya mkononi – hususan simu za kiganjani na vifaa
vya mawasiliano vya kiganjani (tablets) – vina namba maalum
inayovitambulisha. Namba hiyo inajulikana kama IMEI ambacho ni kifupi
cha International Mobile Equipment Identity.
Kifungu cha 84 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta
(EPOCA) ya 2010 kinataka kuwepo kwa mfumo wa rajisi ya namba za
utambulisho wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi. Rajisi hii inajulikana
kwa kiingereza kama Central Equipment Identification Register, kwa
kifupi CEIR. Sheria inataka rajisi hiyo ihifadhiwe na kuendeshwa na
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.
Aidha Kanuni za mwaka 2011 za EPOCA kuhusu mfumo wa rajisi ya namba
za utambulisho wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi inawataka watoa
huduma wa mawasiliano yanayotumia vifaa vya mkononi kuweka mfumo wa
kudumu wa kumbukumbu za namba tambulishi (Equipment Identity Register –
EIR) za vifaa vya mkononi vinavyotumika kwenye mitandao yao.
Mfumo huu wa kielektroniki ambao utahifadhi kumbukumbu za namba
tambulishi za vifaa vya mawasiliano vya mkononi una lengo la kufuatilia
namba tambulishi za vifaa vinavyoibiwa, kuharibika, kupotea au ambavyo
havikidhi viwango vya matumizi katika soko la mawasiliano.
Vifaa vyote vya mawasiliano vya mkononi ambavyo vimeibiwa,
vimeharibika, kupotea au visivyokidhi viwango vya matumizi katika soko
la mawasiliano havitaweza kufanya kazi kwenye mitandao ya mawasiliano
kutumia vifaa vya mkononi.
Zifuatazo ni Faida za Rajisi.....
1. Kutambua Simu kama ni Feki au Laa
Kujenga misingi ya matumizi ya simu halisi, zisizo bandia. Mtumiaji
ataweza kutambua iwapo simu aliyo nayo inakidhi viwango, ni halisi na
sio bandia.Simu feki za kiganjani ambazo hazina viwango na ubora zina athari kubwa kwa watumiji kiafya. Kwa watu wanaotumia simu ambazo hazikidhi viwango vya ubora zinaweza kuwaletea madhara kwenye ubongo. Athari hizo huonekana taratibu hivyo ni vigumu kwa watu kugundua kwamba wanaathiriwa kwa namna moja au nyingine.
2. Kuzibiti wizi wa simu.
Iwapo mtu atapoteza au ameibiwa simu ya
kiganjani na akatoa taarifa kwa mtoa huduma, simu hiyo itafungiwa
isiweze kutumika kwenye mtandao mwingine wowote wa simu za kiganjani.
Mteja anaponunua simu ni lazima adai risiti halali na halisi na pia
garantiii ya angalau miezi 12. Mteja anatakiwa aihifadhi risiti hiyo
angalau kwa miezi mitatu. Baada ya hapo, iwapo simu imekuwa inatumika,
taarifa za matumizi zinaweza kutumika kama uthibitisho mbadala wa milki
ya simu husika.
3. Kuhimiza utii wa sheria:
Kifungu cha 128 cha EPOCA kinamtaka mtumiaji
wa simu kutoa taarifa ya kupotea au kuibiwa kwa simu au laini ya simu.
Kifungu cha 134 kinayataka makampuni ya simu kutokutoa huduma kwa simu
ambayo imefungiwa. Mara tu mteja anapopoteza
simu yake ya kiganjani anatakiwa kutoa taarifa kwa kituo cha Polisi cha
karibu ambapo atapewa namba ya kumbukumbu ya taarifa ya tukio, maarufu
kama RB.
Anatakiwa aende kwa mtoa huduma kutoa taarifa ya tukio akiwa na hiyo
RB na uthibitisho wa umilki wa simu iliyopotea ( risiti aliyopewa wakati
wa kununua iwapo itakuwepo). Mtoa huduma kwanza atahakiki umilki wa
simu iliyopotea au kuibiwa na atampatia mteja namba ya kumbukumbu kwamba
simu hiyo imefungiwa isitumike kwenye mitandao ya simu na hatimaye
ataifungia simu hiyo ndani ya saa 24.
Playstore
TeknoTaarifa Video
TAARIFA ZILIZOSOMWA SANA
-
Kwa wale Rafiki zangu wa ma-gadgets and all that... wanaopenda vitu Vikalii. Hii ndiyo orodha ya simu ambazo zimetambulika kuwa...
-
KAIMU KATIBU MTENDAJI BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA Dkt. Charles E. Msonde. TAREHE: 16 JULAI 2014 TAARIFA YA MATOKEO...
-
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amesema serikali imeamua kufanya jitihada hizo baada ya kubaini kut...
-
nimekusanya list ya vitu 5 ambavyo kwa nchi za wenzetu kama Marekani, Ujerumani, Hispania, Ufaransa na Bangladesh pamoja na sehemu nyingine ...
-
Mambo vipi Rafiki yangu? Kama wewe ni miongoni mwa watu wanaopendelea kuweka Pattern kwenye simu zenu kwa usalama zaidi, Basi msijali...
-
Kwa kawaida wajasiriamali wengi hasa wadogo wadogo huzingatia mipango ya kukuza mitaji, kuimarisha uwezo wa wafanyakazi, kukuza faida, k...
-
Kampuni ya simu nchini China ya Huawei yatoa tarakilishi zilizo na mtandao wa interneti kwa shule kadhaa magharibi mwa Uganda. Hatua hi...
-
Cocaine ilionaswa Polisi wa Ufaransa wamemkamata afisa mmoja wa kukabiliana na mihadarati ...