Baskeli hii imetengenezwa na wataalam wa Formula 1 wakishirikiana na Chuo kikuu cha Lughborough cha Uingereza. Chuo kikuu cha Loughborough ni chuo kikuu bora katika michezo nchini Uingereza kwa zaidi wa miaka 20 mfululizo.
Bei ya Baiskeli hiyo ni Shilingi milioni 52 za Kitanzania, unaweza kujenga nyumba ya kisasa au kufungua duka zima la baskeli au ukanunua BMW 1 Series mpya kabisa na kubakiwa na chenji, lakini kwa baskeli aina ya Beru factor 001, unapata baskeli moja tu, tukiachana na bei hivi ndivyo vikorokoro vinavyopatikana katika baskeli hiyo.
Fremu ya Beru Factor 001 imetengenezwa kwa malighafi aina ya carbon fibre monocoque ambayo hutumika kutengenezea gari za Formula 1, malighafi hii inaifanya baskeli kuwa na umadhubuti wa hali juu na uzito mdogo sana. Bila ya kutia chumvi unaweza kuinyanyua baskeli hii kwa kidole kimoja tu lakini hautaweza kuipinda hata ukiamua kuigonga kwa nyundo nzito! kikubwa utachuna rangi tu.
Wanunuaji wa baskeli hiyo hutengenezewa kwa mujibu ya maumbile na uwezo wao wa kuendesha baskeli. Mteja hutakiwa kwenda maabara za Chuo kikuu cha Loughbough kufanyiwa uchunguzi wa afya na maumbile ili atengenezewe baskeli hiyo. Wataalam sita huchukua muda wa wiki nzima kukamilisha utengenezaji. Baiskeli hiyo tayari umeshawekwa katika makumbusho ya kisayansi nchini Uingereza kutokana na ubora wake.