Facebook ambayo kwa sasa inapatikana katika lugha 70 ulimwenguni, ni
mtandao wa jamii ambao unaongoza kwa kuwa na watumiaji wengi zaidi
duniani. Wewe na mie kama watumiaji wa Facebook tunainufaisha kampuni
hiyo ya Facebook, kwani kupitia kuitumia kwetu kunaiwezesha Facebook
kuingiza mapato kwa njia ya moja kwa moja au nyingine.
Makala hii inakuchambulia namna ambavyo Facebook inaingiza "vijisenti" vyake:-
1. Kupitia Matangazo: Kwakuwa inao watumiaji wa mtandao wengi, ni
rahisi kwa Facebook kushawishi watu binafsi na makampuni kutangaza
bidhaa zao kupitia aina mbalimbali za matangazo yanayorushwa hewani na
Facebook. Mfano , kampuni inaweza kudhamini POST yake, ili ionekane kwa
watu wengi zaidi na mara nyingi. Pia kuna matangazo ya biashara ambapo
unaweza kutengeneza tangazo lako la biashara na kulirusha hewani kupitia
Ukurasa wako wa Facebook (Facebook Page). Ili kutengeneza tangazo
Facebook, unaweza kuenda sehemu maalum ukiwa Facebook imeandika CREATE AN AD.
Unahitaji kuwa na Credit Card au Umejisajili na unayo akaunti ya Paypal ili kuweza kulipia huduma hii.
Mfano wa matangazo yanayoingizia Facebook 'vijisenti' |
Namna nyingine kampuni ya Facebook inavyoingiza 'vijisenti' |
2. Salio maalum la Facebook ( Facebook Credit)
Ni kama vile unavyonunua salio la simu yako ili utumie salio hilo kupiga simu, ila kwa Facebook, unaponunua Facebook Credit,
ni kwa ajili ya kuweza kutumia credit hiyo kulipia kucheza Games, au
hata kununua vitu katika baadhi ya maduka yanayouza bidhaa zao ndani ya
Facebook.
Unahitaji kuwa na Credit Card au Umejisajili na unayo akaunti ya Paypal ili kuweza kununua Facebook Credit.
Sehemu ya Games ndani ya Facebook, baadhi ya Games inabidi ulipie, na unaweza tumia Facebook Credits kulipia. |
3. Kupitia Kuudha bidhaa mbalimbali
Facebook inayo huduma ya kuuza bidhaa mbalimbali kwa mtindo wa "Gift"
ambapo wewe mtumiaji unachagua nani unataka kumnunulia bidhaa , kisha
unaenda kwa profile ya huyo unayetaka kumuuzia bidhaa. Utaona sehemu
imeandikwa GIVE GIFT, ukibofya hapo utakutana na aina mbalimbali za
zawadi na maelekezo. Hata hivyo huduma hii ya kutoa zawadi kwa watu
haipataki kwa kila nchi. Inabidi ucheki Profile ya mtu husika unayetaka
kumpa zawadi kuona kama GIVE GIFT ipo katika profile yake.