Header ads

Header ads
» » Ndoa ya lazima kwa wachumba watakokutwa faraghani usiku Indonesia

Ndoa ya lazima kwa wachumba watakokutwa faraghani usiku

Sheria mpya ya kuwaozesha vijana watakaokutwa pamoja faraghani baada ya saa tatu usiku nchini Indonesia

Serikali ya mkoa wa West Java nchini Indonesia imeweka sheria mpya ya kuwafungisha ndoa wachumba wachanga watakaokutwa pamoja faraghani baada ya saa tatu usiku.
Mkuu wa mkoa alisema kwamba walinzi wa usalama watatekeleza hatua hiyo ili kuepukana na visa vya ngono miongoni mwa vijana kabla ya kufunga ndoa.
Mkuu wa mji wa Purwakarta Dedi Mulyadi, alihutubia wakazi 200 wa mji katika mkutano wa baraza uliofanyika siku ya Jumatatu na kutangaza rasmi sheria hiyo mpya.
Akibainisha azma yake ya kutaka kudumisha utamaduni na maadili miongoni mwa vijana, Dedi alitoa tahadhari ya kuadhibiwa kwa watu watakaokiuka sheria hiyo.
Machifu wa vijiji waliunga mkono sheria hiyo huku mmoja wao akifahamisha kuwahi kutekeleza hatua hiyo hapo awali.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post