Jiji la Durban ni mojawapo ya miji iliyopo katika pwani ya Afrika Kusini.
Uamuzi huo ulitolewa baada ya mkutano mkuu uliofanywa na maafisa wa mashirika ya kufanikisha tamasha hiyo ya michezo nchini New Zealand.
Mkuu wa shirika la CGF Prince Tunku Imran alisema “Ni ufahari mkubwa kwa Afrika baada ya Durban kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa michezo ya 22 ya Commonwealth”.
Michezo ya Commonwealth hufanyika kila baada ya miaka nne na wanariadha hutoka kwa zaidi ya nchi 50 wengi wao wakiwa raia wa nchi zilizokuwa chini ya ukoloni wa Uingereza.
Michezo ya Commonwealth kwa mara ya kwanza yalifanyika mwaka 1930.