Huduma ya mawasiliano ya WhatsApp Web iliyokuwa ikitumika kwenye simu za Android, Windows Phone na Black Berry sasa pia imeingizwa kwenye simu za iPhone.
Watumiaji wa simu za iPhone wataweza kuunga programu zao za WhatsApp kwenye tarakilishi kwa kutumia huduma hiyo ya WhatsApp Web.
Ili kuweza kuanza kutumia huduma ya WhatsApp Web, watumiaji wa simu za iPhone wanatakiwa kuingia kwenye sehemu ya kitufe cha mipangilio na kuichagua katika programu zao za WhatsApp.
Wakati huo huo, watapaswa kufungua tovuti ya web.whatsapp.com kwenye tarakilishi zao na kuunganisha simu kwa kutumia kisimbuzi cha kodi ya QR.