Basi moja itazinduliwa mnamo Alhamisi na katika siku zijazo mabasi mengine yataongezwa.
Ingawa basi hiyo itatumia gesi, nishati inayotumika katika shughuli kama vile kuongeza nguvu katika beteri na katika vyombo vya mawasiliano na televisheni kwenye basi itazalishwa na paneli za jua zilizoko katika sehemu ya juu ya basi hiyo.