Tumezoea vitu vingi sana kutengenezwa katika umbo la miraba minne au mstatili na si katika simu tuu. Hii ni kwenye tableti, milango , madirisha, TV, na vitu vingine vingi tuu. Ila hakuna aliyewahi kufikiri umbo la duara au mviringo jinsi gani litakuwa kwenye kifaa kama simu janja.
Kuna simu ya kwanza kabisa yenye umbo la duara kutengenezwa itaingia sokoni hivi karibuni. Simu hiyo inaitwa Runcible, na inatengenezwa na kampuni ndogo huko Marekani.
Kwa nini wameamua kutengeneza simu ya umbo la mviringo?
Kwa kifupi mwanzilishi wa kampuni ya Monohm inayotengeneza simu hizi Bwana Heorge Arriola
anadai lengo kuu ni kuleta utofauti katika kizazi ambacho simu zimekuwa
zikiwafanya watu wengi zaidi kutofurahia maisha ya kila siku nje ya
simu zao. Yaani milio ya taarifa fupi (notifications) kutoka mitandao ya
kijamii kwenye simu na tableti zao zinawafanya watu watumie muda mwingi
zaidi wakitazama simu zao kuliko kufanya mazungumzo na watu waliokaribu
nao.
Kiubunifu
wamechagua umbo hili kutoka kwenye saa ambazo kwa muda mrefu zilikuwa na
umbo la duara zaidi na pia kutoka kwenye umbo la dira yaani ‘compass’
ambazo kwa miaka mingi mamia kwa mamia zimekuwa zikitengenezwa katika
umbo la mduara.
Je nini cha kitofauti?
Kwanza
kabisa simu hii itakuwa inatumia programu endeshaji (OS) ya Firefox OS,
hii ni OS mpya inayotengenezwa na kampuni ya Firefox.
Pili,
ili kukuepusha wewe kupoteza muda sana katika mitandao ya kijamii kila
baada ya kutumia taarifa fupi yaani ‘notifications’ wao wataondoa hili
na kufanya ‘icon’ yaani ile sehemu ya kubofya kufungua app husika kuongezeka ukubwa kila unapotakiwa kupata taarifa fupi.
Kwa hiyo njia pekee ya wewe kutaka kujua kama kuna ‘notifications’ mpya
itabidi utazame kioo cha Runcible, hii itasaidia kwani kumbuka hakutakuwa mlio wala mtetemeko (vibration) pale unapokuwa na ujumbe mpya katika mitandao ya kijamii.
Tatu, itadumu miaka na miaka! Kivipi? – Wametengeneza katika hali ambayo vifaa mbalimbali vya ndani kama vile kamera, RAM, na vingine vingi kuweza kubadilishwa ili kuongeza uwezo wake na hivyo kuondoa ulazima wa wewe kununua mpya kisa ina uwezo mkubwa zaidi wa RAM, kamera na mengineyo. Wenyewe wanadai wanataka simu hii iweze kupita kwenye familia kizazi kwa kizazi
Nne, je ujapenda muonekano flani wa vazi lake (cover)? Nalo utaweza badilisha kiurahisi tuu.
Umbo
lake sio kubwa sana na unaweza kuiweka kwa urahisi mfukoni, kwenye
shati au suruali n.k. Pia utaweza kuunganisha na kamba ya mvuto au cheni
kama ukitaka.
Ungana nami Ili uwe unazipata taarifa toka kwangu Bofya hapa kwa FACEBOOK
Ungana nami Ili uwe unazipata taarifa toka kwangu Bofya hapa kwa FACEBOOK