Wanafunzi 7 wa kitivo cha uhandisi wa mashine cha chuo kikuu cha Uludag nchini Uturuki wamefanikiwa kuunda gari la kutumia nishati ya umeme linaloweza kuendeshwa kwa kasi ya kilomita 90 kwa saa moja kwa matumizi ya mwezi mmoja pekee.
Gari hilo aina ya ULUMAK lenye nafasi ya kubeba abiria wawili limegharimu fedha lira 25,000 katika uundaji.
Gari hilo limeweza kufanyiwa majaribio kwa mafanikio katika hatua 3 tofauti.
Gari hilo linaloweza kuingizwa chaji kwa masaa 8 linaweza kusafiri kwa masafa ya kilomita 70.
Gari hilo lina uzito wa kilo 400, urefu wa mita 3.4 na upana wa mita 1.6.
Wanafunzi hao waliarifu lengo lao la kutaka kuboresha gari hilo na kubadili tena muundo wake ili lifikie hatua ya kuweza kutumika.
Wanafunzi hao pia walitoa wito wa kuomba msaada kutoka kwa viongozi.
Chanzo: .topgear.com