Nyota huyo amebakiza mkataba wa mwaka mmoja wa kubaki TP Mazembe inayokataa kumuuza kwenda kucheza Ulaya.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Samatta alisema kuwa ndoto zake hivi sasa amezielekeza kwenda kucheza soka la kulipwa na siyo Afrika.
Samatta alisema kufikiria kurejea kucheza ligi kuu ya nyumbani ni kujirudisha nyuma kimaendeleo, hivyo amepanga kuzitimiza ndoto za kuondoka Mazembe mwakani mara baada ya mkataba wake kumalizika. “Ujue kila mchezaji ana malengo katika kupata maendeleo ya soka na wengi wao ni kupata mafanikio ya kucheza soka la kulipwa Ulaya.
“Hizo ndizo ndoto nilizozipanga, sitaki kurudi nyuma, badala yake kusonga mbele, hivyo nimepanga kurejea kucheza soka hapa nchini baada ya miaka ishirini,” alisema Samatta.