Tuko hospitali ya mkoa wa Njombe muda huu.Mimi Niko kichochoroni nimejibanza baada ta kuanza kupigwa mabomu na polisi.
Wananchi walifunga njia ili kuishinikiza serikali itoe tamko juu ya mauaji ya RAIA aliyeuawa kwa risasi na polisi bila hatua.
Wananchi wametawanyika hovyo hivyo nitawajuza baadae kinachoendelea huko barabarani. Hapo jana iliripotiwa Polisi kuua Mwananchi kwa Risasi saa tatu usiku kwa kosa la uzurulaji=> Polisi waua raia kwa risasi Njombe kwa kisingizio cha uzurulaji
==== Updates =====
Wagonjwa walioko mawodini hali ni mbaya,moshi wa mabomu ya machozi umeleta athari kubwa sana.Manesi na madaktari wanahangaika kukimbia hakuna Huduma yoyote inayoendelea hapa hospitali.


