Ushindi wa leo dhidi ya Juventus ya Italia, umemaanisha kuwa kocha Luis Enrique ameivunja rekodi ya Pep Guardiola ya kuzoa makombe matatu katika msimu wa awali klabuni hapo.
Goli la kwanza la Barcelona lilifungwa mnamo dakika ya tano ya mchezo baada ya Rakitiç kumalizia pasi safi kutoka kwa Iniesta.
Goli hilo lilidumu hadi mapumziko
Morata alirudisha matumaini ya Juventus baada ya kusawazisha goli hilo punde tu walipotoka mapumziko.
Kusawazishwa kwa goli hilo kulinyanyua ari na morari ya Barcelona ambayo iliwatumia vyema Suarez na Neymar kupigilia misumari mingine miwili.
Hongera kwa Barcelona ambao ni mabingwa wapya wa klabu bingwa barani Ulaya maarufu kama UCL.