
Bugatti Veyron Super Sports ndio gari iliyo ghali kuliko zote Duniani ambapo
gari hiyo imeuzwa moja tu kwa toleo la mwaka 2012. Tuanze na bei gari hii toleo
la Super Sports ni US$ 2,400,000 sawa na Shillingi za Tanzania karibu trilioni
tatu nukta tisa.

Kwa upande wa kasi gari hiyo ina
uwezo wa kutoka 0 hadi 60 kph kwa muda wa sekunde 2.5 na pia hufikia kasi ya
200 kph kwa muda wa sekunde 7.3 yaani muda huu ni kuanzia kuwa gari imesimama.
(kutoka sifuri). Kasi ya ya juu kabisa ya gari hiyo ni 430 kph, yaani ina kasi
kuliko hata gari za Formula One.


Buggati Veyron Super Sports ina injini yenye kutumia lita
nane na ina silinda kumi na sita, injini hiyo ina jumla ya maredieta kumi kwa ajili
ya kuipoza. KWa upande wa nguvu injini Buggati Veyron ina jumla ya horse power
1,2000 na turbo charger nne. Gari hii pia ina double difusser exhast system.
Buggati Veyron ina uzito wa karibia tani mbili (1.8)
Kwa upande wa gia; gari hii ina dual clutch, yaani
ukitaka unaweza kuiendesha kama manual na ukipenda unaweza kuiendesha kama
automatic, ina tanki la mafuta lenye uwezo wa kuingia jumla ya lit 100. Barani
Afrika gari hii bado haijawahi kununuliwa.