Leo tutatizama njia za kuifanya
computer yako ifanye kazi kwa kasi na kupunguza matatizo ya hapa na
pale. Hii ni maalumu kwako kama unatumia platform yoyote ya Windows,
iwe Windows 7, 8 au 8.1. Haijalishi kama computer yako ni ya bei ghali
sana, ina processor na RAM kubwa lakini kama utendaji kazi wake ni wa
kusuasua haina maana sana.
Labda computer yako huchelewa sana
kuwaka au kufungua mafaili. Au inaganda na kujiwasha upya pasipo sababu
ya msingi unayoifahamu. Usihofu, mambo yafuatayo ni muhimu kwako kama
unaijali computer yako. Unaweza pia kusoma computer bora kwa ajili yako
na laptop bora za mwaka 2014.
Nimeandaa hii kwa kuunganisha
Windows 7 na 8, Windows 8 haina Start button hivyo tumia sana sehemu ya
Search pembeni mwa screen yako.
- ZUIA PROGRAMU ZINAZOFUNGUKA PINDI UNAPOWASHA COMPUTER.
Programu
zote za computer zimetengenezwa katika njia ambayo huziwezesha
kujifungua punde tu computer inapowashwa. Mara nyingi hautaweza kuziona
kama zimeshafunguka kwa sababu zinajifungua nyuma ya pazia na bila wewe
kujua. Utaona computer yako ikionesha tu kuwa iko busy. Programu hizi
kwa kiasi kikubwa huchangia kuifanya computer yako itumie nafasi kubwa
kuzihudumia. Zuia program usizozihitaji zifunguke kila mara unapowasha
computer. Ili kufanya hivo;
- BONYEZA kwenye keyboard vitufe hivi kwa wakati mmoja Ctrl + Shift + Esc.
- Subiri kidogo baada ya muda itafunguka Task Manager. Angalia katika vipengele vyake na chagua sehemu iliyoandikwa Start Up. Hapo utaona list ya program zote zinazofunguka punde unapowasha computer yako. Utaweza kuona uzito wake kuna None. Low, Medium na High.
- Zuia program usizozihitaji hasa zitakazo kuwa na Medium na High.
- TUMIA PERFORMANCE TROUBLESHOOTER YA WINDOWS.
Microsoft wakati wanatengeneza
window hujua kabisa kwamba matatizo yatatokea. Na saa nyingine matatizo
ambayo hayagunduliki kwa urahisi na mtumiaji. Hivyo katika computer yako
kuna program ya Performance Troubleshooter. Hii hutafuta na kurekebisha
matatizo mengi katika utendaji kazi wa computer yako automatically. Ili
kuitumia Performance Troubleshooter;
- FUNGUA> Control Panel (Windows 7 inapatikana kupitia Start, Windows 8 elekeza mshale wa kipanya katika upande wa chini kuchoto kisha Right Click sio Left Click unaweza Search - Control Panel)
- Ukishafungua Control Panel, andika Troubleshooter katika search box.
- Kisha bonyeza Troubleshooting
- Chini ya System and Security mwishoni bofya Check for Performance Issues (Windows 8 chagua Run Maintainance Tasks).
- SAFISHA COMPUTER YAKO KWA CCLEANER
Nimewahi kuzungumzia CCleaner katika post yangu ya Programu 10 za muhimu
kwa ajili ya computer, hii programu ni nzuri sana katika kutunza
computer yako. Ni ya bure ingawa baadhi ya huduma zake za advanced
unaweza kuhitajika kulipia. Bure ni nzuri pia. Tumia hii kusafisha
computer yako na pia kusafisha Registry. Pia unaweza kutumia kufuta
sehemu zisizokuwa na kitu (kama mapengo) katika hard disk. Download CCleaner hapa.
- FUNGUA PROGRAMU CHACHE KWA WAKATI MMOJA
- RESTART COMPUTER MARA KWA MARA.
Hii itasaidia kutumia RAM yako vizuri. Unapowasha computer yako data
zote zinatunzwa katika RAM. Hivyo ukitumia computer kwa muda mrefu mambo
mengi yatachukua nafasi katika RAM yako. Unapozima computer RAM hufuta
data zote na ukiiwasha RAM huwa safi na kuweza kutumika tena. Lakini pia
computer ina tabia ya kupata joto sana. Joto sio rafiki mzuri wa kifaa
chochote cha chuma hivyo ukiizima na kuiwasha kidogo inapoa.
- ZIMA BAADHI YA VISUAL EFFECTS.
Tulia. Usichanganikiwe na mambo. Hapa panahitaji umakini wako kidogo.
Visual Effects hizi ndizo zinaifanya windows iwe na muonekano fulani.
Visual Effects huipa windows muonekano wa kuvutia. Lakini hizi hunyonya
nguvu nyingi ya computer pia. Hivyo ninakushauri kutumia njia hii kama
computer yako imeelemewa sana na shughuli. Ili kuzima baadhi ya Visual
effects;
- FUNGUA - Control Panel
- Kisha search Performance Information and Tools. Kisha katika list chagua tena Performance Information and Tools. (Windows 8, unaweza kusearch moja kwa moja Performance Information and Tools kupitia Search kulia mwa screen yako, chagua Settings kupata majibu).
- Bonyeza Adjust Visual Effects, ingiza password yako administrator kama ikihitajika.
- Bonyeza kipengele cha Visual Effects, bofya Adjust for Best performance kisha bonyeza OK. Kama wewe sio mtaalamu sana hapa chagua tu Let windows choose what's best for my computer. Kisha Bofya OK.
Shukrani kwa kuendelea kutembelea blogu yetu hii. Ukipata tatizo lolote
usisite kunitumia ujumbe. Maoni na ushauri yanakaribishwa pia.