Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara (Mb.) ametuma salamu za rambirambi kwa Baraza Kuu la Waislamu Nchini (BAKWATA) na Waislamu wote nchini kufuatia kifo cha Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Shaaban Issa Bin Simba kilichotokea Jumatatu, tarehe Juni 15,2015 katika hospitali ya TMJ Jijini Dar es Salaam alipokuwa anatibiwa.
Katika
salamu hizo, Mhe. Mukangara amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kumpoteza
kiongozi huyo ambaye bado Taifa lilikuwa likimuhitaji hasa katika kipindi hiki
cha kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba
mwaka huu.
Waziri
huyo ameongeza kuwa Mufti atakumbukwa kwa upole
, unyenyekevu wake na kutopenda makuu,wakati wa uhai wake marehemu alikuwa
tayari kumsikiliza kila mtu bila kujali dini au kabila lake.
“Nimepokea
kwa huzuni nyingi taarifa ya kifo cha Sheikh
Mkuu wa Tanzania Mufti Shaaban Issa Bin Simba ambaye alikuwa Kiongozi
anayeshirikiana vizuri na viongozi wote wa serikali na vyama mbalimbali katika
kuhakikisha Watanzania wanaendelea kuwa wamoja” amesema .
Amesema Waziri
Mukangara: “Nakutumia salamu zangu za rambirambi wewe Katibu Mkuu, BAKWATA na
waislamu wote nchini na naungana nanyi katika kuomboleza msiba huu mkubwa
katika nchi yetu.
Aidha,
kupitia BAKWATA, natuma salamu za dhati ya moyo wangu kwa familia ya marehemu
kwa kumpoteza mpendwa wao. Napenda wajue kuwa msiba wao ni msiba wangu. Pia,
naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aiweke pema
peponi roho ya marehemu … Amina.”
Imetolewa
na;
Idara ya
Habari(MAELEZO)
15 Juni,2015