Header ads

Header ads
» » Jengo laanguka na kuua watu nne (4) nchini China

Watu wengine 3 wajeruhiwa katika janga lingine mjini Zunyi ndani ya juma moja

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa vyombo vya habari ,watu wanne wamefariki baada ya jengo kuanguka katika mji uliopo kusini magharibi nchini China.
Kwa taarifa kutoka katika gazeti la Shaghai miili ya waliokufa imepatikana baada ya timu ya uokoaji kufanya jitihada za uokoaji kwa muda wa masaa 15 katika mji wa Zunyi.

Gazeti hilo linaendelea kusema kuwa bado inaaminika kuwa bado watu 20 wamebaki ndani ya majengo 9 ya kihistoria katika mtaa wa Honghuagang na wengine 3 kujeruhiwa.
Uchunguzi unaendelea kufanyika kujua sababu ya kuanguka kwa jengo hilo,huku wanaowajibika na kuanguka kwa jengo hilo watachukuliwa hatua kali.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post