Klabu ya Yanga itamkosa mshambuliaji
wake, Mrisho Ngassa katika msimu wa ligi kuu na mechi za kimataifa
mwakani kufuatia habari za mchezaji huyo kusaini kuchezea klabu ya Free
State ya Afrika ya Kusini kwa miaka mitatu.
Klabu hiyo ilimtaka
mchezaji huyo mwaka jana kwa dau la dola 80,000 lakini klabu yake
ilitaka ilipwe dola 150,000. Ngasa alionesha ishara ya kuiaga klabu
Yanga katika sherehe za kukabidhiwa kombe la ligi kuu Tanzania Bara
baada ya kuvua jezi zake na fulana yake ya ndani ikisomeka “ I will
always love Yanga, Thanx, Bye” akimaanisha kuwa ataipenda Yanga siku
zote katika maisha yake, asante, kwaheri Yanga.Ngasa aliwahi kufanya majaribio katika klabu kadhaa ikiwemi Timu ya West Ham ya Uingereza mwaka 2009 ikiwa chini ya kocha Zola lakini hakufanikiwa. Vyombo vya habari vimeripoti kuwa Ngasa atajiunga rasmi na timu hiyo mwezi July akiwa mchezaji huru. Ngasa ameisaidia Yanga kutwaa ubingwa na amekuwa mfungaji na kiungo muhimu katika kusababisha magoli