Bunge
la Tanzania limepitisha muswada wa sheria ya udhibiti wa ajira za
wageni wa mwaka 2014 ,ambapo pamoja na mambo mengine unaainisha
vipengele muhimu vya ajira kwa wageni na wazawa.Hata hivyo bunge hilo
limesisitiza serikali kupitia taarifa za waomba ajira wageni ili kubaini
uwezo kuhusu ajira wazoomba na mienendo yao kijamii.
Sheria hiyo
pia inawataka watanzania kuwepo katika ajira zote kutokana na sifa
zao.huku wageni wakianishiwa aina ya ajira kulingana na mahitaji ili
kuleta ushindani sahihi katika soko la ajira nchini humo.Sheria hiyo inalenga kuvutia waombaji wenye ujuzi kutoka nje kulingana na mahitaji,huku pia ikitoa fursa kwa wazawa.Akichangia muswada huo kabla ya kupitishwa mbunge wa Karatu Yohana natse anaeleza jinsi wazawa wanavyopaswa kunufaika zaidi
Gaudensia Kabaka ni waziri wa kazi na ajira wa Tanzania na hapa amesema kuwa vibali vya kazi kwa wageni na suala la uraia kwa mjibu wa sheria hiyo ni mambo ambayo hayataenda pamoja,bali kinachotakiwa ni kutumiza masharti yote mawili.