Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.
William Vangimembe Lukuvi akipewa na Mkurugenzi Mkuu wa NHC maelezo ya
uendelezaji wa eneo la Usa-river lililonunuliwa na NHC kwa ajili ya
kujenga Jiji la kisasa hapo jana.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.
William Vangimembe Lukuvi akiondoka eneo la Meru Residential arpatments
alipomaliza kukagua nyumba za makazi zilizojengwa na NHC na kuuzia
wananchi hapo jana.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akimweleza
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe
Lukuvi juu ya mpango wa NHC wa kujenga maduka makubwa ya kibiashara ili
kuhudumia wananchi na wakazi walionunua nyumba za makazi za Meru
alipomtembeza Waziri huyo hapo jana
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.
William Vangimembe Lukuvi akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa
nyumba na kuingia ndani kukagua nyumba hizo.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu
akisalimiana na wafanyakazi wa NHC waliokuwa wamejipanga kumpokea Waziri
Lukuvi kufungua nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani
Longido.
Hizi ni nyumba za gharama nafuu zilizokamilika kujengwa
na NHC Wilayani Longido na ambazo ziko tayari kuuzwa kwa wananchi.
Ufunguzi wa nyumba hizi ulifanywa jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu
akikagua maandalizi ya ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa
na NHC Wilayani Longido, Arusha kabla ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi kufanya ufunguzi huo
jana.
Mbunge wa Longido Mhe. Lekule Laizer akilishukuru
Shirika la Nyumba kwa kuiweka Wilaya ya Longido katika awamu ya kwanza
ya utekelezaji wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC
katika Halmashauri mbalimbali za Wilaya hapa nchini.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.
William Vangimembe Lukuvi akihutubia halaiki ya wananchi wa Longido
(hawapo pichani)waliohudhuria ufunguzi alioufanya wa nyumba za gharama
nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Ntibenda akilishukuru
Shirika la Nyumba kwa kujengwa nyumba Wilayani Longido eneo ambalo ni
kame na lenye changamoto kubwa ya kutekeleza ujenzi wa nyumba bora
Watendaji wa Wizara ya Ardhi Mkoani Arusha na wananchi
wakifuatilia matukio ya ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa
na NHC Wilayani Longido jana.
Mkuu wa Wilaya ya Longido Bw. Ernest Kahindi alitoa
nasaha zake wakati wa ufunguzi rasmi wa nyumba za gharama nafuu
zilizojengwa na NHC Wilayani Longido jana.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akitoa
maelezo kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William
Vangimembe Lukuvi ya mradi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa
Wilayani Longido.
Wananchi wa Wilaya ya Longido wakifuatilia kwa makini
hotuba mbalimbali zilizotolewa wakati wa ufunguzi wa nyumba za gharama
nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani Longido
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.
William Vangimembe Lukuvi akikagua vyumba mbalimbali vya nyumba bora
zilizojengwa na NHC Wilayani Longido.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.
William Vangimembe Lukuvi akifungua rasmi nyumba za gharama nafuu
zilizojengwa na NHC Wilayani Longido. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa
Arusha Mhe. Daudi Ntibenda, Mbunge wa Longido Mhe. Lekule Laizer na
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu.
Wafanyakazi wa NHC nao hawakuwa nyuma kumpokea Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi
alipowasili mradi wa NHC Longido kufanya ufunguzi rasmi.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mikoa na Utawala wa NHC Bw.
Raymond Mndolwa akisalimiana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi alipowasili Longido kufungua rasmi
nyumba za ghrama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani Longido.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu
akimpokea kwa furaha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.
William Vangimembe Lukuvi alipowasili katika mradi wa nyumba za gharama
nafuu za NHC ili kufanya ufunguzi rasmi.
Msafara wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi ukiingia eneo la mradi wa nyumba
za gharama nafuu zilijengwa na NHC Wilayani Longido ili kufungua rasmi
nyumba hizo baada ya kukamilika ujenzi wake.
Hizi ni nyumba za gharama nafuu zilizokamilika kujengwa
na NHC Wilayani Longido na ambazo ziko tayari kuuzwa kwa wananchi.
Ufunguzi wa nyumba hizi ulifanywa jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.
William Vangimembe Lukuvi akikagua nyumba za makazi zilizojengwa na NHC
eneo la Levolosi Jijini Arusha.Nyumba hizi zinauzwa kwa wananchi.Picha zote na Muungano Saguya- Longido, Arusha.