Mwanamuziki nguli wa Hip Hop, nchini kutoka Mwanza, Fareed Kubanda ‘Fid Q’ (kulia) akipozi na Balozi wa Umoja wa Ulaya pamoja na baadhi ya washindi wenzake wakati wa hafla hiyo.
Kupitia kurasa za mitandao ya kijamii mwanamuziki nguli wa Hip Hop, nchini kutoka Mwanza, Fareed Kubanda ‘Fid Q’ Amepongeza kwa kutunukiwa tuzo ya maendeleo 2015 inayotolewa na Umoja wa Nchi za Ulaya .Fid Q alieleza kuwa, kutunukiwa huko ni baada ya mchango wake kuonekana ikiwemo kutoa elimu kwa watoto wa mitaani na vijana kupitia mashairi.
Tuzo hiyo iliyotolewa Machi 17, alipewa kwa sababu maisha yake yanaendana na uhalisia na watu wengine ikiwemo kusaidia jamii akiwa kama msanii na kutambua mchango wake kwa watu wengine.
Mwanamuziki nguli wa Hip Hop, nchini kutoka Mwanza, Fareed Kubanda ‘Fid Q’ (katikati) akiwa na Balozi wa Umoja wa Ulaya, Filiberto Sebregondi (kulia) wakati wa halfa ya kukabidhiwa tuzo hiyo.
Fid Q amekuwa akifanya darasa lililokuwalikijulikana kama UJAMAA DARASA kwa vijana wa mitaani na wanaofanya vitendo viovu vya matumizi ya madawa waliweza kujifunza na kuachana na mambo maovu ya awali.Ambapo amesema pia kwa sasa atarejesha pia darasa hilo kwa vijana kwani pia muziki wake umekua ukielimisha vijana wengi zaidi na watoto wa mitaani.
Fid Q ni miongoni mwa wasanii wakubwa waliosaidia muziki wa Hip Hop hapa Nchini kuendelea kukua zaidi huku watu wa rika zote wakiukubali muziki wake huohasa katika mistari yake iliyojaa vina vya maarifa vya kumsaidia mwanadamu yoyote Yule hapa Duniani, hivyo kwa kutunukia tuzo hiyo amefuraahia na kushukuru wote wanaendelea kumuunga mkono na kumsapoti.
Alichokiandika Fid Q kwenye ukurasa wake wa Instagram.