
Kiungo wa kati wa Southampton Mugubi Wanyama
Kocha
wa Arsenal Arsene Wenger anapanga kumnunua kiungo wa kati wa
Southampton Mkenya Victor Wanyama na mshambuliaji wa Anderlecht
Aleksandr Mitrovic kulingana na gazeti la the Sun nchini Uingereza.Wenger amejiandaa kutoa kitita cha pauni millioni 30 kwa wachezaji hao wawili,huku Wanyama akigharimu kitita cha pauni millioni 20 naye mshambuliaji huyo wa Anderlecht Mitrovic akigharimu pauni millioni 10.
Inaaminika kuwa Wanyama ataondoka katika kilabu ya Southampton iwapo atachukuliwa na kilabu kikubwa huku naye Mitrovic akiwa amekuwa akifuatiliwa na waajiri wa Arsenal katika kipindi cha wiki chache zilizopotea.
Mitrovic amekuwa akifananishwa na Didier Drogba kutokana na mchezo wake.
USISAHAU KUUNGANA NAMI FACEBOOK