Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe na Mbunge wa Viti
Maalum, Al Shaymar Kweigyr wakiongoza matembezi ya hamasa ya kupiga vita
mauaji ya albino nchini yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam kuanzia
viwanja vya Biafra mpaka Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, Mbunge wa Viti Maalum, Al
Shaymar
Kweigyr, Balozi wa Harakati ya Imetosha, Henry Mdimu, Mwakilishi wa Chama cha Albino Tanzania (TAS), Abdillah Omar sambamaba na wadau wengine wakishiriki kuimba wimbo ‘Tanzania Tanzania’ kabla ya kuanza kwa shughuli nzima ya hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini, iliyofanyika jana kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es salaam.

Mbunge
wa Viti Maalum, Al Shaymar Kweigyr akicheza muziki wa sambamba na
Mwanamuziki wa Reggae, Jhiko Manyika “Jhikoman” wakati wa shughuli nzima
ya hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini, iliyofanyika jana
kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es salaam.Kulia ni
Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network ambao ni wadau wakubwa wa
harakati ya Imetosha, Joachim Mushi.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Maandalizi ya Matembezi ya Hamasa ya kupiga vita mauaji ya
albino nchini (Imetosha), Ally Masoud “Kipanya” akimkaribisha Balozi wa
Harakati ya Imetosha, Henry Mdimu ili kuzungumza na Watanzania
waliofika kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es
salaam.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akitoa hotuba yake na
kauli ya Serikali katika harakati ya kupambana na kupiga vita mauaji ya
albino nchini, iliyofanyika jana kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini
Dar es salaam.