Kukua na Kuongezeka kwa teknolojia , Kumerahisisha mambo na
kuongezeka kwa idadi kubwa ya watu wenye ufahamu duniani hivyo basi hata elimu namna ya
kuipata imebadilika. kwani sasa Unaweza kusoma kwa njia ya mtandao na haulazimiki
kwenda chuoni kila siku au mara kwa mara ilimradi uwe na komputa yenye
intaneti. Ingawa watu wamekuwa wakiichukulia kwa ugumu kidogo
ukilinganisha na kuhudhuria darasani kila siku, wanafunzi wanaosoma kwa
njia ya mtandao wanaonyesha kuridhika zaidi na elimu zao na hufanya
vizuri zaidi kwenye matokeo yao.
Zifuatazo ni faida za Kusoma kwa njia ya mtandao
1. Urahisi wa kusoma
Inawezekana watu
wengi wanapenda kusoma kwa njia ya mtandao hasa hasa nchi zilizoendelea
ni kwasababu ya urahisi wake wa kusoma. Mwanafunzi anapata faida asomee
wapi saa ngapi na lini. Haimaanishi masomo ni mepesi , hii inamaanisha
hautatakiwa kwenda darasani kwa muda maalumu kitu ambacho kinasaidia
watu wenye familia au wanaofanya kazi ambazo zinawabana sana.
2. Uwezo wa kupata masomo kwenye mtandao
Kitu
unachohitaji ni komputa na intaneti tu, hivyo unapata na kuweza kusoma
kitu alichofundisha mwalimu kwa njia ya video, sauti na hata nakala za
maandishi ya kawaida. Mfumo huu unakufanya kurudia kitu kama hujaelewa
na hupotezi kitu, kuliko madarasa ya kawaida mwalimu akishafundisha
ukisahau na kama hukuandika inakuwia vigumu kukumbuka alichokisema au
alichoelezea.
3. Mawasiliano na mwalimu wako
Mwalimu siku
zote anapatikana kwa njia ya barua pepe au simu, hautasubiri mpaka
umfuate ofisini au masaa ya kazi. Vilevile unapata matokeo yako haraka
kwa kuwa kila kitu unakifanya kwa njia ya mtandao. Hivyo inakuongezea
kuwajibika na unakuwa unajua mwenendo wa masomo yako mara baada ya
kumaliza kufanya mazoezi ya somo au majaribio ya somo.
4. Gharama zake ni ndogo
Gharama utakayo
lipa ni ada tu ya mwaka, ambayo inakuwa rahisi kuliko elimu ya kawaida
ya kuingia darasani. Vilevile hutahitajika kulipia vitu kama vitabu,
hosteli, gharama za kujiandikisha n.k