Header ads

Header ads
» » hatua 5 muhimu za kupitia kama unaitaji kumiliki website

Kama wewe ni mfanyabiashara wa kati au juu, basi kuwa na Website ni moja ya vitu vya lazima kwa dunia ya sasa. Takwimu zinaonesha, kuna Watanzania milioni tano wapo online kila siku. Hapa hawajajumlishwa wale walio nje ya nchi.
Kuwa na Website ya kampuni kunafungua milango zaidi kwa biashara yako, kila kona ya dunia inayofikika kwa intaneti, basi website yako inaweza kufika. Kwa kutumia mitambo ya utafutaji (searh engines) kama Google, Yahoo, Bing nk, watu ni
rahisi sana kutafuta wanachokitaka online. Hivyo usipoteze nafasi hii ya kipekee kabisa.

Katika makala za awali, tumeandika sana umuhimu wa website, mambo ya kuzingatia nk, leo hii tutaangalia hatua muhimu za kupitia hadi kumiliki website. Hivyo twende kazi...


1.Andaa bajeti

http://www.hellowallet.com/wp-content/uploads/2015/07/WEB_Accounts.png

Bajeti ni kitu cha awali kabisa kwenye kuendea kuwa na website. Siku hizi teknolojia imerahisishwa, unaweza kuwa na website inayoendana na bajeti yako. Siyo lazima uwe na mamilioni ili uwe na website, hakikisha unajieleza ipasavyo pindi unapowasiliana na watengeneza website ili kuwafahamisha ukomo wa bajeti yako na wao wataweza kukupa website iliyo ndani ya kikomo chako.
Kwa mfano, kuhost website ya kawaida haizidi laki moja ya Kitanzania kwa mwaka,na kutengeneza website ya kawaida pia huanzia laki tatu za Kitanzania kwa kampuni ya kawaida,ingawa wapo wanaochaji chini au zaidi ya hapo. Kwa wamiliki wa makampuni makubwa kama Facebook au Google yanatumia mabilioni kuhakikisha website zao zinakuwa hewani bila tatizo.
Hivyo, bajeti haziwezi kuwa sawa, usiogope kujadiliana na mtengeneza Website yako, kama ukipata kampuni iliyo makini, watakusaidia kufikia malengo.




2. Andaa vitu unavyotaka au wazo la website 

Icono Web Idea by Tsufuru

Website ni sehemu ya kampuni, mara nyingi watu huanzisha kampuni baada ya kuwa na wazo fulani, wazo hili ama linaweza kuwa limetoka kwao moja kwa moja ama ni baada ya kuangalia toka kwa wengine. Hivyo, katika hatua hii, andaa vitu unavyotaka viwemo kwenye website yako pia na orodha ya websites ambazo unapenda vitu fulanifulani toka huko.
Kwa kampuni ya kawaida, unahitaji vitu kama kuhusu sisi, huduma tunazotoa, wasiliana nasi pia fomu ya mawasiliano ambapo mtu anaweza kukutumia maombi ya huduma moja kwa moja online.


3 Tengeneza Website

Katika hatua hii, ambayo nayo ina viji hatua kibao ndani yake, utatengeneza website, ama kwa kutumia timu yako au kwa kuajiri kampuni nyingine. Siku hizi Tanzania kuna makampuni mengi sana yanayojihusisha na utengenezaji wa website, unaweza kugoogle na kuyapata. Teknotaarifa.com ni chaguo murua kabisa juu ya hili.
Pia, unaweza kutumia programu nyingi za bure zinazopatikana online kutengeneza website kama Wix.com. Kitu cha muhimu kwenye hili, hakikisha unatengenezewa Website yenye kukuwezesha kubadili na kuichunga website bila kuwa na utaalamu wowote. Siku hizi kuna programu (CMS) nyingi kama Joomla, Wordpress, Drupal nk ambazo zitakusaidia kwenye hili. Bajeti ya website ya kawaida hucheza laki tatu hadi milioni moja kulingana na ukubwa wa kampuni itakayokutengenezea na aina ya Website unayotaka na pia nini kitakuwemo (features). Kumbuka, sio kila king'aracho ni dhahabu, kuna kamampuni mengi yanayosema watakutengenezea website kwa gharama ya chini, ila siku ya mwisho unajikuta unaishia kujuta.
Kama utaamua kuajiri kampuni, hakikisha umepitia kazi zao walizofanya na kuridhika na ubora wa kazi zao. Pia kama utaweza hakikisha unawasiliana na wateja wao kujua ubora wa huduma zao baada ya kazi kuisha. Kwenye hili, kitu cha muhimu kuzingatia pia, ni juu ya uchungaji na uboreshaji wa website, kwani kuna kipindi website italeta matatizo, je nani ni muhusika? (website Maintenance Service)
Kama wewe ni mmiliki wa biashara ndogo, hakuna haja ya kuajiri mtu wa IT kwa ajili ya hili, hivyo unaweza kuwapa jukumu hili watengenezaji wa website wakusaidie kuichunga website yako na wewe ukaendelea na mambo mengine ya biashara. Ila, kumbuka kutaka taarifa za maendeleo ya website yako (web analytics).


4.Chagua jina bora la website
Octen Web Design Domain Name header

Hii ni moja ya sehemu inayowachanganya wengi mno, wengi wamekuwa wakichanganya na kudhani kwamba jina la website ni lazima liendani na jina la kampuni.Hii siyo lazima, jina la website linaweza kuwa tofauti kabisa na lile la kampuni, ingawa kama litakuwa sawa bila kuleta mkanganyiko ni bora zaidi.Ukweli ni kwamba, majina mazuri mengi tayari yameshachukuliwa, hivyo kuna wakati kama nataka jina la website liendane na la kampuni yako, basi itakuwia ugumu na kukulazimisha kuongeza majina ya ziada ili kulifanya liwe la kipekee.
Jina la website ni roho ya website, kwani ni jina ambalo litasambaa kwenye mitandao na watu wote kulifahamu. Hakikisha jina lako lipo la kipekee, epuka kutumia majina ya website ambayo yana maneno mengi, yenye kuchanganya lugha mbili tofauti, yenye maneno yanayofanana; mfano to, two, 2, II nk. Jina la website lazima liwe linalotamkika kwenye simu na pia lisilo na miambatano mingi.
Mambo mengine ya kuzingatia hapa ni kuepuka kununua jina la Website toka kwa makampuni ya uchochoroni, kwani jina lako ni ruru yako kama hii kampuni itakufa katikati ya safari basi unajiweka kwenye hatihati. Pia, hakikisha jina linasajiliwa kwa kutumia taarifa zako na si za kampuni iliyokusajilia.
Mwisho kabisa, msisitizo ni kuwa, jina la Website siyo lazima liwe jina la kampuni,
Gharama za kununua jina la Website ni shilingi elfu 20 kwa .com, .net elfu 24 kwa .org wakati ile ya .co.tz inaanzia shilingi elfu 25.


5. Chagua wapi pa kuweka Website (Hosting)
image

Baada ya kuchagua jina, na kununua, ingawa wengi hupenda kufanya hatua ya nne na ya tatu pamoja, kinachofuata ni kuchagua mahala ambapo website yako itakaa (Hosting).Siku hizi , gharama za kuhost website zimeshuka sana, gharama ya kuhost website haizidi elfu 60 kwa website ya kawaida, hii ikijumuisha email ya kampuni.
Kwenye kuchagua wapi pa kuweka website yako, kama ilivyo kwenye jina, hakikisha unachagua kampuni inayoeleweka. Hakikisha umetembelea website yao na kuona baadhi ya website zinazohostiwa huko. Tembelea hizi website kabla ya kuamua. Mambo ya kuzingatia hapa ni kama;
-Muda ambao website itakuwa online bila kupata tatizo (Reliability); Ukweli ni kuwa, haiwezekani mitambi ikaka mwaka mzima bila kuleta hitilafu hata siku moja, hivyo hakikisha hizi hitilafu sio nyingi,
-Muda wanaotumia kutatua hitilafu (Maintainability); hakikisha, wanatatua tatizo haraka iwezekanavyo kunapotokea hitilafu na huduma kurudi kwenye mstari.
Vitu hivi, unaweza kuvipata kwa kuwasiliana na wamiliki wa website zilizohostiwa kwao au kwenye mkataba wa makubaliana ya huduma (SLA).

Hadi hapo utakuwa tayari una website inayofanya kazi, na sasa unaweza kuiweka kwenye kadi na matangazo ya biashara yako na kuwaambia wateja. 


Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post