Kulingana na Jonathan Mativo ambaye ni msimamizi wa teknolojia hiyo, wahudumu wa afya katika jamii huwasajili wanawake na watoto wao kwa kutuma ujumbe mfupi ambao unawafikia wakuu wa afya katika hospitali wanazosimamia.
Mutivo aidha amesema kuwa wahudumu hao wameekabidhiwa simu za mkononi na kila mmoja anapaswa kuhudumia nyumba ishirini katika eneo analotoka ambapo hunakili hali ya usafi, ripoti za kliniki kwa kila mwanamke mjamzito na watoto wao huku wakiandikisha pia lishe bora kwa watoto, utoaji wa vyandarua vya umbu kwa kina mama wajawazito na watoto wachanga.
Huduma hiyo ambayo Mutivo anasema ni baina ya wizara ya afya ikishirikiana na shirika la Plan international imeenedelea kuwasaidia katika utoaji wa huduma za kiafya vijijini.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na wizara za afya katika kaunti za Pwani ni asilimia hamsini pekee kati ya tisini ya wanawake katika maeneo ya mashinani wanaotembelea kliniki kupimwa wakiwa wajawazito jambo ambalo anasema limechangia kuzaliwa kwa watoto wasiokuwa na afya bora huku wengine wakikumbwa na matatizo ya uzazi.
Kwa upande wa wanawake wanasema kwamba tangia wahudumu hao kuanza kuanza kufanya kazi vijijini, imekuwa rahisi kwa kina mama wengi waliowajawazito kujisajili katika na hata kupata huduma za afya huku wakisema kuwa wahudumu hao pia huwaarifu madaktari mapema iwapo kuna mama anayehitaji huduma za dharura.
Kina mama hao aidha wameongeza kuwa visa vya kina mama kuaga dunia na hata kupata shida wakati wa kujifungua vimepungua kwani wahudumu hao hutuma ujumbe katika zahanati na baadaye hospitali hiyo hutuma gari la kuwasafirisha kina mama hao hadi hospitali tayari kuoata matibabu ya dharura.
Kwa upande wake tabibu katika hospitali ya Mnarani, Mary Kanze ametoa wito kwa serikali kukumbatia teknolojia hiyo ili kupunguza idadi ya watoto wanaozaliwa nyumbani pasi na ambao mama zao hawajakuwa wakitembelea kliniki mara kwa mara huku akisema kuwa kulingana na takwimu za shirika la afya duniani idadi ya kina mama wanaoaga dunia kufuatia matatizo ya ujauzito.
Aidha kina mama pia wameitaka serikali kusimamia mradi huo ili kuhakikisha kuwa mwanamke aliyemjamzito anapata huduma zilizobora.