Miaka
kadhaa iliyolipa umaarufu wa timu hii ulikuwa “noisy neighbours” kwa
maana ya kwamba wana kelele dhidi ya wapinzani wao wa jadi Manchester
United lakini hawana uwezo wa kushinda makombe, hiyo ni Manchester City
ya zamani. Man City ya leo ikimilikiwa na tajiri wa petroli Sheikh
Mansour Bin Zayed Al Nahyan wa ukoo wa ufalme wa Abu Dhabi ni moja kati
ya klabu tajiri Ulimwenguni. Fedha za Man City zinaonekana katika
seahemu mbali mbali, ampabo klabu hii ni moja kati ya klabu zinazolipa
mishahara mikubwa na kununua wachezaji ghali mno. Pia klabu hiyo hivi
karibuni imepitisha mpango wa kuupanua uwanja wa Etihad kufikia kuwa na
uwezo wa kuchukua washabiki 62,000 kwa msimu wa 2015-16, hii itaufanya
Man City kuupiku uwanja wa Emirates na kuchukua nafasi ya pili kwa
ukubwa nyuma ya wapinzani wao Man United.
Chumba cha wachezaji |
UPANDE WA TEKNOLOJIA
Kwa
upande wa teknolojia Man City sasa hivi ni klabu inayoongoza
ulimwenguni, tutayataja baadhi ya mambo yanayoifanya klabu hiyo kuwa na
nafasi hii. Jambo la kwanza ni WiFi. Mwaka jana Man City wamefuata nyayo
uwanja wa Anfield wa Liverpool, Bernabéu wa Real Madrid na Nou Camp wa
Barcelona za kuweka WiFi ya kasi uwanjani, kasi ya WiFi ya Etihad
imevunja rekodi kwa kuwa na uwezo wa mpaka 72Mpbs, tofauti na za
Liverpool, na viwanja vingine ambazo zimeripotiwa kuwa na matatizo
watumiaji wengi wanapotumia sambamba. WiFI hii inawaruhusu wale wenye
app zinazoonyesha kandanda moja kwa moja kama vile SkySports App iliyoko
kwenye gajeti za iOS na Android kuweza kuona marudio ya sehemu muhimu
za mchezo kama vile magoli, penalti, kadi nyekundu moja kwa moja.
Uwanja wa Etihad |
Etihad
pia imewekewa teknolojia ya ghali zaidi ya mstari wa goli, teknolojia
hiyo ni Hawk Eye Spy Cam hugharimu £250,000.00 (Tsh. 686,500,170.00) na
huweza kumuarifu refa mpira unavuka mstari wa chaki ya goli, hivyo
kuondoa utata iwapo refa na wasaidizi wake hawana uhakika wa hili. Hawk Eye Spy Cam inatumika na klabu
zote za ligi kuu ya Uingereza kwa sasa. Mbali na teknolojia hii Meneja
wa Man City anatumia software ya hali ya juu aina ya
Prozone Analysis tool kufanya uchambuzi wa utendaji (performance) wa
wachezaji wake mazoezini na kwenye mechi za Etihad, si ajabu wanapokuwa
Etihad Man City huwa hawashikiki.
Vile
vile Man City imewekeza pound milioni mia moja (Shilingi trilioni mbili
nukta saba nne) kujenga akademi ya kisasa ya mazoezi ambayo itakuwa na
jumla y a viwanja 16, akademi hiyo inatarajiwa kuwa tayari mwanzoni mwa
msimu ujao. Man City pia wataanza kuvaa fulana maalum mazoezini ambazo
zitakuwa zinatoa taarifa za msukumo wa damu, mapigo ya moyo, maji
anayopotezwa mwilini na kiwango cha CO2 anachotoa mchezaji. Sambamba na
fulana hizo Viatu vya wachezaji wa Man City vitakuwa vinatoa taarifa
kama vile mshindo wa mpira (impact) mchezaji anapoupiga, idadi ya hatua
anazokimbia mchezaji kwa kila mechi au mazoezi na taaarifa zote za
kipedometa, kocha ataweza kung’amua kwa urahisi ni nani ana juhudi ziada
au anategea.
Teknolojia
nyingine ambayo tayari iko njiani ni Sisco System StadiumVision ambayo
inatumiwa na timu ya mpira wa kikabu ya Brooklyn Nets ya Marekani. Hii
itaruhusu watazamaji kuona marudio muhimu sehemu za mechi katika pembe
mbali mbali kwa kutumia gajeti zenye WiFi, hivyo kuona video ya mechi
hakutategemea tena kulipia app ya Sky Sports na app nyingine kama
hizo.Hudumua hii itakuwa ni ya kulipia.
Chanzo: foxsports.com