Header ads

Header ads
» » Teknolojia inavyozingatiwa kuandaa viongozi bora Barani Afrika


CHANGAMOTO ya kuwaendeleza vijana kitaaluma nje ya nchi imezidi kuongezeka hivyo viongozi ndani na nje ya nchi wapo katika jitihada kutatua kero zilizopo. Moja kati ya harakati za kuwasaidia vijana ni pamoja na kuanzishwa kwa harakati za kuwawezesha vijana kuandaliwa kuwa viongozi bora wa Afrika wa baadaye (Yali). Yali ilianzishwa na Rais wa Marekani Barack Obama.
Kupitia mpango huo vijana wanafundishwa masuala ya uongozi na kuunganishwa kwa mtandao. Kwa mwaka huu msichana Mtanzania Joan Avit ambaye amejikita katika teknolojia ya Habari na Mawasiliano alichaguliwa kwenda kujifunza kwa wiki sita nchini Marekani. Mwanadada huyu alianzisha programu ya GramoGame App ambayo inamwezesha mtoto kujifunza katika miaka ya mwanzo ya utoto.
Uanachama wa Yali unajumuisha taasisi ambayo inawakutanisha takribani vijana 1,000 ambao ni viongozi watarajiwa. Mwaka huu wamesafiri kwenda Marekani katika vyuo vikuu nchini humo na vyuo vingine kujifunza stadi za kitaaluma na uongozi. Wanapewa mafunzo katika nyanja tatu za biashara na ujasiriamali, uongozi wa raia au usimamizi wa umma. Mwaka huu suala la mafunzo ya nishati pia litazingatiwa.
Watatembelea maeneo mbalimbali wakiwa nchini humo huku wakijifunza kuhusiana na fursa zilizopo katika mitandao ya kitaalamu, huduma kwa jamii na uratibu wa shughuli za kiutamaduni katika kufikia kilele cha kujifunza na kubadilishana tamaduni. Lakini jambo lingine muhimu ni namna ambavyo vijana watakavyohitimisha mafunzo kwa kukutana na Rais Obama jijini Washington DC.

Anasema, ana uzoefu katika fani za kujitolea hasa baada ya kufanya hivyo kwa miaka mitatu tangu akiwa mwanafunzi na baada ya kumaliza chuo kikuu. Kwa mujibu wa Joan, baada ya kumaliza chuo kikuu alifanya kazi za ujasiriamali na hasa kwenye ubunifu wa mradi wa teknolojia.
“Tangu awali nilikuwa na shauku ya kuleta mabadiliko katika maisha ya watoto kwa njia ya teknolojia, hali ambayo ilipelekea kupewa kitita cha Dola za Kimarekani 20,000 kutokea mradi wa Tigo change makers,” anasema Joan.
“Fedha hizo ziliniwezesha kuwafikia watoto zaidi ya 3,000 katika maeneo ya vijijini na hivyo kupunguza ugumu wa kielimu waliokuwa wanakabiliwa nao, ” anasema. “Juhudi zetu za kuelimisha watoto zilifikia hatua ya mafanikio wakati nilipoingia katika mashindano ya programu kidijitali ya Tigo Change-maker na kushinda dola za Kimarekani 20,000 ambazo ni zaidi ya Sh milioni 42 “ anasema Joan.
“Nilitumia fedha hizo katika kuhakikisha kuwa ninanunua na kusambaza vifaa vya kujifunzia kwa watoto zaidi ya 4,200 katika shule zaidi ya 20 wilayani Moshi na baadhi ya shule katika wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro,” anasema.
Joan anasema, msaada kutoka programu ya kidijitali umewawezesha kuzifikia shule nyingi. “Ninafurahia kuwa sehemu ya mabadiliko hayo jambo linalonivutia zaidi ni kuona kuwa harakati zangu hizi zimebadilisha mwelekeo wa ufaulu wa watoto shuleni,” anasema.
Programu hizo za michezo zinafungwa kwenye vifaa vya watoto ili wacheze na wakati huohuo wanajifunza hivyo kuwezeshwa kufundishwa namna ya kusoma. Joan anasema, kwa sasa watoto wanaonufaika na mradi huo wa GramoGame App wanapata fursa nzuri ya kujifunza kwa urahisi namna ya kusoma.
“Lengo letu kwa baadaye ni kuhakikisha kuwa tunafikia mikoa mingi zaidi ya kitanzania ili kuwawezesha watoto wa kila mkoa kusoma,” anasema. Anatoa mwito kwa vijana nchini kuhakikisha kuwa wanajishughulisha kuleta mabadiliko katika jamii walipotoka. 

Chanzo: thecitizen.co.tz

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post