Header ads

Header ads
» » Toyota inatarajia kuzindua Gari la Mbao aina ya Sersuna

 

Teknolojia hii imetokea wapi?

Huko nchini Japan kuna mahekalu ya kitamaduni ambayo huvunjwa na kujengwa upya kila baada ya miaka 20. Kitu cha pekee katika ujengaji wa hekalu hizo no utumiaji wa mbao usiohusisha utumiaji wa ata msumari mmoja katika ujenzi wake.

Teknolojia hiyo inatumika kwa miaka mingi katika ujengaji wa hekalu maarufu Japan – The Ise Grand Shrine

Ubomoaji na ujengaji wa mahekalu hayo umekuwa ukifanyika kwa takribani miaka 1,300 sasa, na huwa wanabomoa na kujenga tena ili kuhakikisha majengo hayo yanaendelea kuwa na nguvu na usalama. Teknolojia ya ujengaji huo inapitia kwa vizazi hadi vizazi, na sasa Toyota wanatumia teknolojia hiyo katika utengenezaji wa gari.
 The Setsuna concept car (Picture Toyota)

Wiki ya Ubunifu mjini Milani, Italia


Takribani mwezi kuanzia sasa kutakuwa na maonesho ya ubunifu katika jiji la Milani, (Design Week in Milan, Italy) na ndio Toyota wanategemewa kutambulisha gari hilo rasmi litakalotambulika kama Sersuna.’

Ubunifu wa gari hilo ambao wameuita Setsuna, unaonesha kitu ambacho wanaweza kukifanya baadae. Wanashiriki maonesho hayo ili pia kuweza kupata mitazamo kutoka wabunifu wengine.

Aina kadhaa za mbao zimetumika kutengeneza bodi la gari hilo, chasis, viti, uskani (steering wheel) na rim za matairi.
The designer and the engineer (Photo Bertel Schmitt) 
Picha ya designer na the engineer wa gari ilo (Picha: Bertel Schmitt)

Je mbao hizo zimejishakaje kama misumari na ‘screw’ hazijatumika?




gari la mbao
mfano: Maumbo ya Convex na Concave

Ni uunganishaji wa sehemu zinazokutana kwa kutumia maumbo ya ‘concave’ na ‘convex’ (umbo la mbonyeo) ndio vinavyoshikanisha sehemu mbalimbali za gari hilo.

CHANZO: forbes.com
MHARIRI: Abdallahmagana.com

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post