Header ads

Header ads
» » Nipime App: Maktaba inayowawezesha wanafunzi kusoma kwa njia ya Simu

Nipime app ni application ya simu iliyobuniwa na wanafunzi vijana wa Tanzania ikiwa na lengo la ufanikishaji wa Elimu kupatikana kwa urahisi bila kujali muda au mahali alipo mwanafunzi. Hii ilitokana na kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi ambao wanakosa mtu wa kuwasaidia pale wanapokuwa mbali na shule au mwalimu, na pengine mzazi hana uwezo wa kumsaidia mwanae katika somo husika.
Hilo ndio lilikuwa wazo la kwanza katika kuanza kubuni Application hiyo.

Walioshiriki katika uundaji wa application hiyo ni :-

 
Elizabeth Ferdinand   - Editor
Oliver Mgongolwa      - Editor
Mackriner Siyovelwa  - Editor
Bless Mgongolwa       - Designing and programming
Pamoja na kushirikiana na walimu wa shule mbalimbali katika kupata mwongozo wa maswali na Summarry mbalimbali.

Pia wabunifu wa application hii walipata nafasi ya kuonesha ubunifu wao katika maonesho yaliyoandaliwa na wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi, yaliyofanyika dara mwaka 2015, na walipata cheti cha ushiriki.
Nipime app ni application ya simu inayomuwezesha mwanafunzi wa sekondari kufanya majaribio (quizzes) katika masomo mbalimbali kama Physics, Mathematics, Biology, Chemistry, Geography, Kiswahili na mengine mengi.
Pia mwanafunzi anaweza pata summary, definitions, laws na shot notes kupitia simu yake ya kiganjani. Mpaka sasa kuna zaidi ya definitions 1000+ katika masomo ya o level.
Mambo mengi katika application hii ya nipime hayahitaji huduma internet baada ya kuinstall na kuiACTIVATE, hivyo basi hata kama ukiwa hauna bando unaweza fanya mengi zaidi. 

Pia application hii inaweza mfundisha mwanafunzi baadhi ya mambo kama jinsi ya kufanya quadratic equations na jkutafuta molar mass kwenye chemical formula mbalimbali.

Kuipata application hii ingia Google Play Store, kisha tafuta Nipime.
Au kupitia link hii --:: edumek.com/getnipime

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post