Mawasiliano yanamchango mkubwa sana katika ukuaji na uendelezaji wa biashara. Hii inatokana na kwamba mawasiliano hutumika katika maeneo mengi hususani kwenye shughuli za kibiashara za kila siku. Kutokana na ukuaji wa teknolojia matumizi ya simu za mkononi na mtandao wa intaneti vimekuwa ni msaada mkubwa katika kuwafikia wateja wengi na wadau mbalimbali wa biashara kwa muda mfupi. Matumizi sahihi ya teknolojia ya mawasiliano yanasaidia ufanisi wa biashara.
Makala
hii inaeleza kwa undani maeneo muhimu na ni namna gani unaweza kutumia
fursa hii kabambe na ya pekee ili kuongeza tija kwenye biashara yako.
Masoko.
Huu ni moyo wa biashara yoyote kwasababu ukuaji wa biashara unategemea
soko kwa kiasi kikubwa. Kutokana na ukuaji wa teknolojia wafanyabiashara
wengi wanatafuta masoko kupitia teknolojia ya mawasiliano kama vile
mitandao ya kijamii mfano whatsup, facebook , linkedin na instagram
ambapo kufanya matangazo ya bishara ni bure au ni kwa bei nafuu. Pia
kama mfanyabiashara unaweza kuuza bidhaa au huduma mtandaoni ambapo
unaweka bidhaa yako mtandaoni pamoja na taarifa zote muhimu kama bei,
mawasiliano na namna gani mteja anaweza kuipata bidhaa au huduma yako.
Hivyo
kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano sio lazima wateja waje sehemu
yako ya biashara ili waweze kupata bidhaa au huduma kutoka kwako, mfano
mzuri wa biashara za mtandaoni ni kama vile kupitia maduka ya mtandaoni
kama kaymuu, ebay na alibaba ambapo mteja anaweza kuagiza kitu kutokea
popote pale duniani na akapata hiyo bidhaa. Njia hii inasaidia kupata
wateja wengi hivyo kuongeza mauzo na hatimaye kukuza biashara yako.
Utunzaji wa kumbukumbu.
Wahenga wanasema, ’’mali bila daftari hupotea bila habari’’. Msemo huu
unaonesha umuhimu wa kutunza kumbukumbu ndani ya biashara kwa kuwa
utunzaji wa kumbumbuku unakusaidia kuona mwenendo wa bishara yako na
kulipia malipo mbalimbali ikiwemo kodi ya mapato ya serikali.
Kutokana
na ukuaji wa teknolojia utunzaji wa kumbukumbu za biashara
umerahisishwa kwani unaweza kufanyika kupitia mfumo maalumu wa
kidigitali (Record Keeping software) ambao una msaidia mjasiriamali
kutunza kumbukumbu za biashara yake kwa haraka na kiurahisi.
Mfumo
huu unaotumia kompyuta ni rahisi na salama kabisa. Pia mfanyabiashara
anaweza kutunza kumbukumbu kwa kutumia mashine za utoaji stakabadhi za
kielektroniki (Electronic Fiscal Device) ambapo mjasiriamali anapaswa
kuitumia kuwapatia risiti wateja wake na kwa kufanya hivyo kumbukumbu
zinajitunza kwenye mashine na inakua ni rahisi kulipa kodi ya serikali
kwasababu taarifa zitakazopatikana ndani ya mashine zinatumika kukadiria
mapato kwa ajili ya kulipia kodi ya ongezeko la thamani kwenye bidhaa.
Hii pia inasaidia kuepuka gharama zisizo za msingi zinazoweza kusababishwa na makosa ya kihesabu.
Manunuzi.
Ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasilianao una mchango mkubwa sana
katika kufanya manunuzi ya malighafi kwa mjasiriamali na hata manunuzi
ya bidhaa kwa wateja. Mfano mzuri wa manununzi kupitia mitandaoni ni
uwepo wa maduka ya mitandaoni kama vile kariakoo shops, ebay na alibaba
haya yote ni mfano wa maduka machache ambayo yapo kwenye mtandao.
Uwepo
wa huduma hii unarahisisha ufanyikaji wa manunuzi kupitia mtandao.
Hivyo unaweza kuwasiliana na wagavi na hatimaye kupata malighafi bila
wewe kusafiri. Aina hii ya manunuzi imeshamiri sana katika biashara ya
kisasa. Inasaidia kuokoa gharama za kifedha na muda pia.
Huduma kwa wateja.
Utoaji
wa hudama bora kwa wateja umeboreshwa kwa kiasi kikubwa. Hii imetokana
na urahisishwaji wa mawasilaono baina ya mfanya biashara na mteja ambapo
imekuwa ni rahisi kufuatilia kama bidhaa imefikia mteja na kupata
mrejesho kutoka kwa mteja baada ya matumizi ya bidhaa na kujua kama kuna
maboresho yoyote yanayohitajika.
Vilevile
matumizi ya teknolojia ya mawsiliano na habari imefanya kuwepo kwa
mahusiano ya karibu kati ya mfanyabiashara na mteja kwani imekuwa ni
rahisi kufanya mawaisiliano. Hata kama mteja akiwa mbali na biashara
ilipo uwezekano wa kufanya mawasiliano umekuwa ni mkubwa sana na kwa
gharama nafuu zaidi.
Pamoja na hayo
imeonekana kuwa wajasiriamali wengi wanashindwa kutumia fursa hizi kwa
sababu mbalimbali. Baadhi wanakumbana na changamoto ya matumizi ya vifaa
vya Teknolojia ya mawasili kama vile simu za kisasa na kompyuta, huku
wengine wanaofahamu matimizi yake wanachukulia kama gharama na upotevu
wa muda hivyo kutupilia mbali fursa hii. Hata hivyo ukweli utabaki kuwa
ukweli kwamba teknolojia ya habari ni mkombozi na wale wanaotumia
teknolojia hii wanaendelea kuonesha utofauti na kuwa mfano bora katika
soko. Hivyo basi ni vizuri kila mjasiriamali anayetaka kufanikiwa aweze
kuchukua hatua inayostahili ili kuboresha huduma kwa wateja, kudhibiti
gharama na kuleta mabadiliko katika biashara na soko kwa ujumla.
Chanzo: smallbusiness.chron.com