Header ads

Header ads
» » » Jinsi ya kuokoa simu iliyoingia maji kwa kutumia Mchele


Ulikuwa umeishika vibaya na ikakuponyoka na kuangukia kwenye beseni..au kwenye dimbwi la maji… au kwenye sehemu ya kuogelewa (Pool).. Hizo ni baadhi tuu ya maeneo ambayo yanaweza sababisha simu au tableti yako kukutana na maji. Jambo ambalo linaweza sababisha kufa kwa kifaa chako cha bei nono!
Mara nyingi jambo la kwanza atakalofanya mtu ni kuhangaika kufuta maji hayo mara moja…. iwe kwa kutumia nguo yake, au chochote kile cha karibu. Ila je ni sahihi? HAPANA!
 

Hatua ya 1: Image titled Save a Wet Cell Phone Step 1
Itoe mara moja kwenye maji. Inavyozidi kukaa kwenye maji muda mrefo ndivyo uwezekano wa kupona katika janga hili unakuwa mdogo zaidi. Imedondoka kwenye choo? Hapo itakubidi ufanye maamuzi ya haraka kama utaichomoa haraka au uisahau kabisa. Utafanya nini?
 

Hatua ya 2: Image titled Save a Wet Cell Phone Step 3
Bila kupoteza muda izime mara moja! Na kama ni simu yenye eneo la kutoa betri basi usitumie switchi yake kuzimia, bali toa betri mara moja. USIJARIBU KUBONYEZA KINGINE CHOCHOTE, ONDOA BETRI. Na kama ni tableti au simu za iPhone ambazo hazina sehemu za kutolea betri bofya eneo la kuzimia mara moja.

LENGO: Ni kuzima simu au tableti hiyo kabla hakujatokea shoti ya aina yeyote, kama simu imeingia maji alafu ukaifuta na kuanza kujaribu kuichezea kwa kubofya unaweza sababisha shoti inayoweza ikaiua simu yako mara moja

. Hatua ya 3: Image titled Save a Wet Cell Phone Step 6
Ifute taratibu. Kwa kutumia kitu kama taulo lililo kavu, angalia kwa ukaribu maeneo kama vile ya kuweka waya wa ‘earphones’, hakukisha pameacha kutoa maji. Puliza maeneo ya matundu kuhakikisha maji yameisha kabisa ndani. Pia toa vitu kama vile kadi ya laini, memori kadi na betri, kava, vikaushe pia.

Usitumie njia za ajabu kama vile kuiweka kwenye oveni ili kuikausha…joto la oveni ni kali sana utaua simu yako.
 

Hatua ya 4:
 
zungushia simu yako kwenye tishu (Toilet Paper/Napkins) kisha iweke kwenye chombo ulichoweka mchele wa kutosha kuifunika kabisa. Mchele unasifa ya kunyonya unyevunyevu. Unazungushia tishu ili kuondoa uwezekano wa simu yako kuingiwa na vumbi la mchele.

 
Hatua ya 5:
Baada ya kufanya tulichoongelea katika hatua ya 4 itakubidi usibiri takribani masaa 32 hadi 72, hapa kipimo ni chako wewe. Kama ililowa kidogo tuu basi masaa 32 yatatosha kabisa, ila kama ililowa sana, basi hakikisha ikae masaa 72. TUNAJUA UTAKUWA UNAHAMU YA KUIWASHA AU KUITOA KABLA, ILA KUMBUKA NI MUHIMU IKAUKE NDANI KABISA, Hivyo vumilia.


Hatua ya 6:

Tunajua baada ya hatua hizo zote utakuwa unasubiria kwa hamu kuiwasha tena. Hadi sasa itakuwa imekauka vizuri ndani, ukiiwasha tunategemea itawaka bila tatizo lolote kama ulifuata hatua zote kwa usahihi.
 

NB: Njia hii inategemea bahati na uharaka wako katika kuondoa simu na kuizima baada ya kuwa katika maji. Kitu muhimu na kuweza kuzima simu au tableti hiyo kabla shoti haijatokea ndani yake
    Ata kama itawaka vizuri na kuweza kufanya kazi kama kawaida kuna uwezekano mkubwa sana simu hiyo kuanza kutofanya kazi vizuri baada ya kipindi kirefu kama vile mwaka mmoja hivi kutokana na madhara ya kuingiwa na maji. Kuna vitu ndani yake huwa havitakiwi kukutana na maji kabisa. Hivyo ata kama itawaka na kuanza kufanya kazi kama kawaida anza kujiandaa kununua simu nyingine.
    Kama simu yako ilikuwa bado ya Dhamana, yaani Warranty basi jua dhamana hiyo imevunjika rasmi. Simu janja nyingi za kisasa zinazouzwa zikiwa chini ya dhamana ya mwaka au miaka miwili zikikupa uwezo wa kuzirudisha na kupewa mpya n.k kutoka pale uliponunua huwa dhamana hizo zinafutwa kama simu iliingia maji. Na wameweka teknolojia spesheli (water indicator) ndani ya simu hizo ambapo kama simu au tableti zikilowa huwa wakifungua ndani wanatambua. 


Chanzo: wikihow.com

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post