Header ads

Header ads
» » Mourinho amewashambulia madaktari wa timu yake kuwa ni 'wajinga'' baada ya kutumia muda mrefu kumtibu Eden Hazard uwanjani

 
 mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Premia ya Uingereza walipokuwa wakikabiliana na Swansea jana usiku huku wakiwa na mchezaji mmoja zaidi yao.
The Blues, ambao tayari walikuwa keshampoteza kipa Thibaut Courtois aliyekuwa kaoneshwa kadi nyekundu kwa kumwangusha mshambuliaji Bafetimbi Gomis walisalia 9 uwanjani baada ya timu ya utabibu kukimbia kushughulikia mguu wa Hazard na wakachukua muda mrefu japo kulingana na Mourinho hakukuwa 'ameumia sana''
''kwa kweli sikufurahia kauli yao ya kumtibu Hazard,ilitulemaza na kuwapa Swansea fursa ya kutushambuliwa maanake walikuwa na watu wawili zaidi yetu'' alifoka the Special one''
 
''Hapa uwanjani uwe ni mbeba mpira, daktari ama hata katibu mwandishi sharti uwe unafahamu jinsi mpira unaendelea uwanjani''
''Kabla ya kuingia uwanjani sharti ufahamu hali halisia kuwa tumekosa mchezaji mmoja na kuingia kutasababisha mwengine aondoke uwanjani''
''Nina hakika Eden hakukuwa katika hali mahututi ilikuwa tu ni kugongwa kidogo ,angeweza kuvumilia,kila mtu alikuwa amechoka '' aliongezea Mourinho
Mourinho alikuwa akizungumzia kisa uwanjani Chelsea walipokuwa nyuma dhidi ya Swansea huku wakiwa na wachezaji 10 kisha Hazard, akaangushwa na Gylfi Sigurdsson.
Wakati huo zilikuwa zimesalia dakika 6 pekee mechi hiyo kukamilika ndipo watabibu wa timu wakaingia kumsaidia walipomuona akichechemaa.
 
Chelsea ndio walikuwa wa kwanza kucheka na wavu kupitia mkwaju wa free-kick uliopigwa na Oscar kunako dakika ya 22 kisha
Andre Ayew akaisawazishia Swansea dakika saba baadaye.
Federico Fernandez alijifunga mwenyewe baada ya kutapatapa na mkwaju uliopigwa na Willian na kufanya mambo kuwa 2-1.

Lakini mambo hayakuishia hapo, Swansea walikuwa na ari ya kuzoa alama zote tatu na juhudi zao zilizaa matunda baada ya kipa wa Chelsea
Courtois kumuangusha Bafetimbi mbele ya lango na refarii akapuliza kipenga akiashiria ni penalti.
Kipa wa mpya wa ziada wa Chelsea Asmir Begovic alijipata uwanjani bila kupenda baada ya Courtois kuoneshwa kadi nyekundu kunako dakika ya 55 ya kipindi cha pili.
Bafetimbi aliihakikishia Swansea alama moja ya kufungua msimu alipofunga na kufanya mambo kuwa Chelsea 2 Swansea 2.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post