Header ads

Header ads
» » Nyota wa Barcelona Lionel Messi aondoka na tuzo mbili za UEFA

Monaco Fußballer Lionel Messi UEFA Preis 2015

Mshambuliaji matata wa Barcelona na kapteni wa Argentina Lionel Messi, amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa UEFA katika msimu wa 2014-2015.
Messi alibeba tuzo hiyo kwa kuwapiku wapinzani wake Luis Suarez na Cristiano Ronaldo waliokuwa wameorodheshwa kuwania tuzo hiyo.

Mshindi wa tuzo hiyo alibainika baada ya shughuli ya upigaji kura iliyotekelezwa hapo jana na wanahabari kutoka nchi 54 zenye uanachama wa UEFA katika ukumbi wa Grimaldi Forum mjini Monaco.
Messi amefanikiwa kupeleka tuzo hiyo nyumbani kwa mara ya pili ikiwa ni pamoja na ile ya kwanza aliyowahi kushinda msimu wa 2010-2011.
Kwa upande wa wanawake, mshindi wa tuzo hiyo alichaguliwa kuwa Celia Sasic aliyewashinda wenzake Dzsenifer Marozsan na Amandine Henry.

Wakati huo huo, Messi pia aliweza kuondoka na tuzo ya goli bora la UEFA la msimu wa 2014-2015.
Goli lililomletea Messi tuzo hiyo lilikuwa ni lile alilolifunga kwenye mechi ya UCL iliyochezwa kati ya Barcelona na Bayern Munich.

Goli hilo liligonga vichwa vya habari kutokana na ufundi wa Messi uwanjani uliomfanya beki wa Bayern Munich Jerome Boateng kutambaa chini.
Kwa sasa swali lililobakia vichwani mwa wapenzi wa soka ni kwama je, Messi ataweza kumpiku mpinzani wake wa karibu Ronaldo kwenye tuzo ya mchezaji bora wa FIFA?

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post