Wanafunzi Sita wa Makerere waunda programu (APP) ya vyakula asilia
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Makerere wapata mafanikio ya kuweza kuunda programu mpya ya vyakula vya asili.
Wanafunzi hao sita wa kitengo cha lishe na chakula,walisema walitengeneza programu inayofahamisha kuhusu lishe na manufaa ya vyakula vya asili hasa katika kanda hiyo.
Programu hiyo kwa jina la 'Sinza' ni ya mfululizo wa video zinazoeleza vyakula mbali mbali vya asilia na vitamini zinazopatikana ndani yake.
Aidha wanafunzi hao kwa majina ya ames Katongole, Bw Bion Solomon, Bi Sarah Mize, Bi Amanda Birungi, Bi Walugaba Shamim na Bi Bugesera Racheal walihojiwa kuhusu ufumbuzi huo na kusema kuwa wanataka watu waelewe kuhusu vyakula vya asilia na lishe bora.
Vile vile walitoa wito kwa wanafunzi wengine kutumia elimu yao kuboresha jamii .
Chanzo: edufrica.com/