Katika utekelezaji wa taratibu
zilizoainishwa katika kanuni za ubora wa huduma za Mawasiliano ya
Ki-Elekronik na Posta za mwaka 2011, (Electronic and Postal
Communications (Quality of Service) Regulations, 2011) Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) imefanya upimaji wa Ubora wa huduma za
Mawasiliano (Quality of Service (QoS) tests) kwa huduma za sauti na
huduma za kimtandao kulingana na mtazamo wa watumiaji wa huduma hizo ili
kuona kiwango cha ubora na uwajibikaji wa watoa huduma za simu za
mkononi pamoja na kuhakiki kiwango cha Ubora wa Huduma wanazo toa kwa
watumiaji wa huduma za simu za mkononi. Taarifa hii inatolewa baada ya
upimaji uliofanyika kuona ubora wa huduma zitolewazo na kampuni ya
Airtel (T) Ltd, Kampuni ya Viettel (T) Ltd inayojulikana kama Halotel,
Kampuni ya Benson Informatics Ltd, inayojulikana kama SMART, Kampuni ya
Millicom International Cellular (T) Ltd, inayojulikana kama Tigo,
Vodacom (T) Ltd na Zanzibar Telecom Ltd inayojulikana kama ZANTEL katika
majiji ya Arusha, Dar es Salaam na Mwanza. Upimaji huo ulifanyika
kuanzia tarehe 1 hadi tarehe 12 Februari 2016 na kuanzia tarehe 7 hadi
tarehe 11 Machi 2016.
Ukaguzi huo ulifanyika katika mifumo ya teknolojia ya 2G and 3G.
Kampuni ya SMART inatoa huduma zake kwa kutumia mfumo wa teknolojia aina
ya 2G pekee katika Jiji la Dar es Salaam. Dar es salaam
Mtandao wa TIGO ndio kinara kwa kuwa na kiasi cha simu chache zilizoshindwa kuunganishwa huku mitandao mingine yote ikishindwa kufaulu jaribio hilo, kwa upande wa simu kushindwa kumalizika mtandao wa TIGO ndio ulikua na simu chache zaidi zilizoshindwa kumalizika ukifuatiwa na VODACOM na HALOTEL. Kwa upande wa jaribio la ubora wa sauti mtandao wa AIRTEL ndio ulio ongoza na ukifuatiwa na HALOTEL pamoja na VODACOM
Mwanza
Kwa mujibu wa majaribio yaliyofanywa na TCRA ni VODACOM pekee ndio walifaulu kigezo cha simu kushindwa kuunganishwa kwa sababu mitandao mingine ilipata idadi kubwa ya simu kushindwa kuunganishwa kuliko idadi inayotakiwa na TCRA, kwa upande wa simu kushindwa kumalizika (yaani simu ambazo zinakatika katikati ya maongezi) VODACOM TIGO na HALOTEL ndio walio ibuka vinara baada kuwa na simu chache ambazo zilikatika katikati ya mazungumzo kama ambavyo grafu inaonesha. Katika upande wa ubora wa sauti katika mtandao wa 3G hakuna mtandao ambao ulifikia viwango vilivyowekwa na TCRA.
Arusha
TCRA inasema kama unaangalia mtandao ambao hauna matatizo ya simu kushindwa kuunganisha katika 3G kwa Arusha HALOTEL ndio imefikia viwango mitandao mingine haikufikia viwango vilivyowekwa na TCRA, na kama unaaangalia mtandao ambao hautakuwa na uwezekano wa simu kukatika katika hovyo basi HALOTEL SMART, TIGO na VODACOM ndiyo mitandao ambayo unaitafuta kwa sababu AIRTEL wao hawakufaulu kiwango kilichowekwa na TCRA. Na kama unatafuta mtandao wenye ubora wa sauti wakati wa maongezi basi SMART ndiyo mtandao pekee uliokidhi vigezo vya TCRA kwa mtandao wa 3G Arusha.
Soma taarifa yote hapa.
Chanzo: TCRA