Header ads

Header ads
» » Teknolojia Imeyaweka Maisha yetu kwenye Mafanikio makubwa

 QuickMobile Promotes Craig Hughes to Vice President of Business Development for Technology Partnership Expansions
Maisha yangekuwa vipi bila teknolojia? Watu wangekuwa wanaishi vipi katika ulimwengu wa sasa kama hatungekuwa na teknolojia hata kidogo? Siku hizi ulimwengu umebadilika kutokana na mabadiliko katika ulimwengu wa teknolojia japo uvumbuzi bado unatolewa kila uchao.
Naomba tuangazie mawasiliano. Wajua tofauti kubwa kati ya wanadamu na wanyama ni kwamba wanadamu wana uwezo wa kuwasiliana kwa kutumia lugha ambayo huwa pengine kwa njia ya kutumia maneno ama ishara. Dhima kuu ya kuwasiliana baina ya wanadamu ni kuuwasilisha ujumbe na kuhakikisha kuwa ujumbe ambao umekusudiwa kuwasilishwa unawasilishwa kwa njia mwafaka bila mushkil wowote.
Hali hii ya uwezo wa wanadamu kuwasiliana inatupa taswira kamili kuwa ulimwengu haungefikia kiwango ambacho umefikia kwa sasa bila njia mwafaka ya kuwasiliana. Kuna vikwazo mbalimbali ambavyo huwazuia watu kuwasilisha ujumbe kwa njia mwafaka na mojawapo wa kikwazo kikubwa ni utofauti katika matumizi ya lugha. Kila mja ana lugha yake ambayo huwa anaitumia kuwasilisha ujumbe na mara nyingi hali hii hutatiza mawasiliano hasa ikiwa pande zote mbili ambazo zinashiriki katika mazungumzo hazitumii lugha moja.

Kwa mfano, ni vigumu kwa mtanzanua ambaye anakifahamu Kiswahili tu kuwasiliana kwa njia mwafaka na mja kutoka marekani ambaye kwake lugha ya Kiswahili ni kama usiku wa giza. Hebu fikiria, hapa kuna waja wawili, mmoja anajua tu kuzungumza Kiswahili na kiingereza kwake ni kitendawili na kuna mwingine ametoka marekani na anakifahamu kiingereza tu na Kiswahili kwake ni kama mazigaombwe na jamaaa hawa wanataka kuzungumza na waelewane pengine kwa ajili ya shughuli za kibiashara, je wataweza kuwasiliana vizuri kweli? Bila shaka hataweza kuwasiliana vizuri. Kwa nini? Kwa sababu ya utofauti wa lugha.

Katika hali kama hii, utafsiri unahitajika na watu wengi huanza kumsaka mkalimani. Wakati mwingine kupatikana kwa mkalimani huchukua muda na pia ni ghali kumlipa mkalimani. Mkalimani pia huchukua muda mrefu na hivyo basi kurefusha mazungumzo na hata wakati mwingine maana hupotea na dhima halisi ya kuuwasilisha ujumbe hupotea.
Lakini hakuna haja ya kukuna kichwa tena kwa sababu teknolojia imerahisisha haya yote kwa kukuletea tafsiri ambayo inatafsiri lugha jinsi ilivyo na bila kupoteza maana na hivyo basi kurahisisha mawasiliano, kubadilishana mawazo na hatimaye kuinua uchumi wa taifa na mataifa.
Tafsiri ya Kiswahili ya Microsoft ni teknolojia ya kisasa ambayo inamwezesha mtumiaji wake kupata fursa ya kutafsiri mazungumzo kutoka katika lugha ya kiingereza hadi katika lugha ya Kiswahili ama na kinyume chake pia bila tatizo lolote. Unashangaa kama hili linawezekana? Ewe! Yote yawezekana na tafsiri hii ya Kiswahili ya Microsoft na ni mufti kiasi kwamba kuna uwepo wa mawasiliano ya moja kwa moja kwa kutumia lugha tofauti lakini kila mmoja anapata ujumbe katika lugha ile ambayo anaielewa.
Tuseme kuna mzungu anataka kuwasilaiana na mtanzania ambaye anaelewa tu Kiswahili kwa kutumia mtandao wa Skype. Katika hali kama hii, mzungu atatumia kiingereza kuwasilisha ujumbe naye mtanzania atapata ujumbe huo katika lugha ya Kiswahili, akishapata ujumbe, atajibu kwa Kiswahili naye mzungu atapata majibu hayo katika lugha ya kiingereza bila maana kupotea na ujumbe kuwasilishwa kwa njia asilia.
Jaribu tafsiri ya Kiswahili ya Microsoft na ujionee, utaipenda na utaishikilia Kikiki.

Na Abdallah Magana

 >>Lengo langu ni kuakikisha upitwi na Habari za Teknolojia ungana Nami FACEBOOK , TWITTER na INSTGRAM

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post