Huawei yaanzisha mafunzo kupitia mtandao wa Interneti katika shule nchini Uganda
Kampuni ya simu nchini China ya Huawei yatoa tarakilishi zilizo na mtandao wa interneti kwa shule kadhaa magharibi mwa Uganda.
Hatua hiyo ilitekelezwa kufuatia kuwa na makubaliano baina ya ICT na serikali ya Uganda ya kuzindua mfumo 'digital' katika elimu nchini humo.
Takriban tarakilishi 30 zilizo na interneti ya Airtel Uganda zimetolewa na kampuni hiyo kwa Shule ya Msingi Kashwa,Rwamkoma na shule ya upili ya Karo zote zilizo katika wilaya ya Kiruhura ncini humo.
Sherehe ya kutoa tarakilishi hizo ziliongozwa na waziri wa ICT John Nasasira ambaye alihimiza umuhimu wa kuwepo kwa elimu kuhusu tarakilishi katika shule za msingi.