Mtandao wa jamii wa Twitter umeboresha vitufe vya ishara maalum (emoji) kwa ajili ya watumiaji katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Emoji hizo zimepambwa kwa ishara ya mwezi pamoja na muonekano wa jengo la msikiti.
Mtumiaji anaweza kuipata emoji hiyo endapo atatanguliza alama ya reli (hashtag) kisha aandike neno Ramadhan (#Ramadhan).
Wakati huo huo, emoji hiyo ya Ramadhan pia imeweza kuboreshwa katika programu ya Periscope.
Chanzo: thenextweb.com/