Akaunti za mitandao ya kijamii ya Twitter na Pinterest za Mwanzilishi wa mtandao wa Facebook Mark Zuckerberg zimethibitishwa kudukuliwa.
Uchunguzi uliofanywa kuhusu udukuzi wa akaunti hizo ulionyesha kuwa hifadhi za data ziliibiwa mnamo mwaka 2012.
Wadukuzi wa bilionea huyo waliweza kusambaza ujumbe wa mafanikio yao ya kuweza kushambulia akaunti zake za Twitter na Pinterest.
Hata hivyo wataalamu wa udukuzi waliweza kurekebisha na akaunti hizo kuwa hali salama tena.
Chanzo: trt.net