Header ads

Header ads
» » Kampuni ya PayPal yatangaza kusitisha huduma zake nchini Uturuki

Kampuni ya PayPal inayohusika na mfumo wa malipo kupitia mtandao imetangaza kusitisha huduma zake nchini Uturuki.
Kampuni hiyo ya Marekani imetangaza kuchukuwa uamuzi huo baada ya kunyimwa kibali na shirika la udhibiti wa huduma za fedha.
Kufuatia uamuzi huo, PayPal itasitisha rasmi huduma zake nchini Uturuki kuanzia tarehe 6 Juni siku ya Jumatatu.
Hivyo basi, wateja wote wenye akaunti za PayPal nchini Uturuki watalazimika kuhamisha fedha zao kwenye akaunti zao za benki kabla ya Jumatatu.
 
PayPal ilitoa maelezo na kuarifu kwamba itaweza kuendeleza huduma zake Uturuki endapo wataweza kupewa kibali cha biashara.
PayPal ni kampuni kubwa inayotoa huduma zake katika nchi mbalimbali zilizoendelea kama vile Marekani, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Uhispania, Ubelgiji, Austria, Uswisi na nyinginezo.

Chanzo: techcrunch.com

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post