Header ads

Header ads
» » » Teknolojia mpya zapitishwa na WHO kwa ajili ya kugundua HIV kwa watoto wachanga



Shirika la afya ulimwenguni, WHO limetoa kibali cha awali kwa teknolojia mbili za aina yake zinazoweza kubaini Virusi Vya Ukimwi, VVU kwa watoto wachanga ndani ya muda mfupi.

Mbinu hizo moja iitwayo Alere™ q HIV-1/2 Detect iliyobuniwa na kampuni ya Alere na ile ya HIV-1 Qual Assay kutoka Cepheid AB zinaweza kubaini VVU kwa mtoto hata chini ya saa moja badala ya kusubiri sampuli kupelekwa maabara ambako yaweza kuchukua wiki au hata mwezi kupata majibu.
Mike Ward kutoka kitengo cha kanuni cha WHO kuhusu dawa muhimu amesema hatua hii ni ya muhimu sana katika harakati za kudhibiti Ukimwi miongoni mwa watoto.
Amesema mbinu hizo ni rahisi, haraka na hazihitaji miundombinu ya hali ya juu kama mbinu zilizopo na zinaweza kutumiwa katika eneo lolote la huduma ya afya.
Kupitishwa kwa mbinu hizo kunafuatia majaribio ya mwaka mmoja na nusu kwa ushirikiano baina ya WHO, Afrika Kusini na Marekani.

Chanzo: unmultimedia.org na UNAIDS/maktaba

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post