Header ads

Header ads
» » Badilisha Akaunti Yako Ya Facebook Kuwa Page kwa Njia Rahisi zaidi

 
Mambo vipi Rafiki zangu wasomaji wa Website hii, Siku chache zilizopita niliulizwa swali na Rafiki yangu toka Chuo cha Mipango- Dodoma.

Swali: Ni Jinsi gani unaweza tengeneza Facebook Page?

Tukiachana na hiyo je ushawahi sikia kuwa unaweza badilisha akaunti yako ya facebook na kuwa page? yaani  watu wakaanza kuku ‘Like’ baadala ya kuku ‘Add As A Friend’. Najua unaweza ukawa na maswali mawili hapo juu ya kwanini na ni kwa vipi?.. Ngoja nikujibu Yote 

Kama inavyojulikana Facebook ni moja kati ya mitandao ya kijamii ambayo inatikisa dunia kwa sasa. Licha ya hivyo pia Facebook wana vipengele vingi sana na bado wanaendelea kutoa vingine vingi ambavyo vinaifanya Facebook izidi kuwa Juu. 

Kwa Nini Ubadilishe Akaunti Yako Ya Facebook Kuwa Page

Kama unatumia ukurasa wako wa facebook kufanya biashara za mtu au hata kutangaza biashara ya mtu si sahihi ni unakiuka vigezo na masharti. Biashara zote inabidi zifanyike katika ‘Page’ na sio akaunti za kawaida kama unazotumia. Kwa kifupi huruhusiwi kutumia ukurasa wako wa facebook kuwasilisha kitu kingine chochote kisichokuwa kinahusiana na wewe kwa mfano biashara yako.
Kutokana na hayo basii unahitaji Page ili utangaze na kuendesha biashara yako. Sasa si vizuri kuanza na moja kabisa. Si unaweza tuu kubadilisha akaunti yako ikawa ndio page yako. Hii itakurahisishia kwa sababu hata watu waliokuwa marafiki zako watakua ndio watu wako wa kwanza kwanza kulike page hiyo
Pia kumbuka Facebook inaruhusu akaunti ya kawaida kumiliki marafiki 5000 tuu lakini ukiwa na page hata kufikisha bilioni inawezekana. Sasa baada ya kujua sababu twende tukajua tutafanikisha vipi jambo hili.

Jinsi Ya Kubadilisha Ukurasa Wako Wa Facebook Kuwa Page

Kabla ya kuchukua maamuzi ya kuendelea ni vyema kujua taarifa gani zitahama kutoka katika ukurasa wako na kwenda samabamba katika Page yako. — Hapa utajua nini kitabaki na nini kitapotea —

Nini Kitahama

– Kama nilivyosema awali marafiki zako wote na followers wako watakuwa ndio watu wanao ‘ like’ page yako
– Username Yako ndio itakuwa username ya Page Yako
– Picha ya kwenye profile lako ndio itakua picha ya kwenye Page yako
– Bado utakuwa na mamlaka sawa katika Page zingine ambazo unaziendesha

Nini Hakitohama/Kitafutika

Post zako, Picha na Album zote hazitakuwa zimehama bali zitafutika hivyo Teknokona inashauri uhifadhi taarifa zako zote kabla ya kufanya zoezi hili
Pia utapoteza cheo chako katika makundi yote ambayo yapo chini yako. Hivi tunashauri kuwa kabla ya kufanya zoezi hili uchague mtu na umeweke awe ndio mwendeshaji wa makundi hayo.
Sasa unaweza kuendelea na kubadilisha akaunti yako ya Facebook kuwa Page kwa kufuata Maelekezo haya.
  • >Log in katika ukurasa wako wa facebook
  • >Fuata (bofya) Link Hii Kuanza kubadilisha Akaunti yako kuwa Page
  • >Chagua Aina ya page unayotaka katika machaguo yaliyojitokeza   
 Convert-Profile-to-Page-Facebook
  • >katika kuchagua aina ya page chagua pia ‘Category’ inayokufaa kisha bofya ‘Get Started’
 Select-Specific-Category

Safii sasa umefanikiwa kubadilisha Akaunti yako ya facebook kuwa page. Ni matumaini yangu kuwa tatizo lolote au ukikwama katika kipengele chochote juu ya makala hii utanishitua Rafiki yangu

 

>>Lengo langu ni kuakikisha upitwi na Habari za Teknolojia ungana Nami FACEBOOK , TWITTER na INSTAGRA

 

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post