Header ads

Header ads
» » Tetesi: Diamond akubali Millioni za Ukawa



LOWASSA VS MAGUFULI

Chanzo hicho kilieleza kwamba, jamaa huyo amekuwa akishawishiwa kujipambanua kuwa atamfanyia nani kampeni kati ya Lowassa na Dk. John Pombe Magufuli wa CCM zitakazoanza Agosti 22, mwaka huu.
“Unajua hata kipindi kile wakati Lowassa anatangaza nia Arusha, jamaa (Diamond) alikwenda kwenye shoo kwa sababu ya mkwanja tu lakini ukweli ni kwamba alikuwa upande wa Bernard Membe (naye alikuwa mtia nia wa CCM).

KWENYE MTONYO
“Unajua Dangote (Diamond) linapokuja suala la mtonyo, huwa halazi damu. Ukweli anaomba Mungu tu mamilioni yatue mikononi mwake maana yeye siyo mwanasiasa ni mfanyabishara kupitia muziki.
“Anakwambia muziki ni biashara kama biashara nyingine. Ni kama kuuza maji, haijalishi wewe ni chama gani lazima utahitaji maji au huduma nyingine yoyote bila kujali siasa,” kilidai chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa gazetini na kuongeza :
“Huo ndiyo msimamamo wa wasanii wengi, Ukawa wakileta mzigo watapatiwa huduma yao na CCM nao wakija watapewa huduma wanayohitaji. Ni kama siti ya daladala, haijalishi anayekalia ni Chadema au CCM.”
KUTOKA NDANI YA UKAWA
kwa mujibu wa Global Publishers, duru za kisiasa kutoka ndani ya Ukawa zilidai kwamba, tayari fungu limetengwa kwa ajili ya wasanii watakaozunguka na mheshimiwa (Lowassa) Tanzania nzima kwa ajili ya kampeni.
“Diamond ni mmojawapo lakini wasanii watakaokuwa bega kwa bega na Lowassa ni wengi. Kuhusu kama wameshasaini mikataba lipo wazi kwani (muda) wowote watadakishwa mamilioni yao,” kilisema chanzo chetu ambacho ni mmoja wa wasanii walio ndani ya Team Lowassa tangu akiwa CCM.

Rais Kikwete akiongea na msanii Naseeb Abdul “Diamond” alipomkaribisha Ikulu kumpongeza kwa kushinda tuzo tano za muziki za kimataifa mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Desemba 23, 2014.
Ijumaa : Oke. Kwanza hongera kwa sababu kuna habari imetufikia kwenye Dawati la Ijumaa kwamba, umevuta mamilioni ya Ukawa. Hii ishu ikoje ?
Diamond : Habari njema hizo. Sijasaini mkataba lakini nazingoja kwa shauku kubwa.
Ijumaa : Nasikia wanakutafuta sana hao Ukawa, je, umeshaongea nao ?
Diamond : Mimi ni mwanamuziki wa Tanzania, nina haki ya kwenda kumburudisha Mtanzania yeyote ikiwa ametimiza hitaji la malipo yanayotakiwa kwa shughuli yake.
Haitakiwi Ukawa wala CCM kunilaumu kwa namana yoyote ninapokwenda kutoa huduma ya burudani.
Mimi napokea simu nyingi za biashara na mimi ni mfanyabishara, kwa nini dili likija nisilichukue ? Dili lije nalisubiria.
URAFIKI WA DIAMOND NA JK

Mara kadhaa Diamond amekaririwa akisema kuwa JK ni rafiki yake mkubwa akimwita Daddy ndiyo maana humtembelea mara kwa mara ikulu hivyo kwa kuwa ni Mwenyekiti wa CCM anaweza kumshawishi msanii huyo kuzunguka mikoani kumpigia kampenzi mgombea wake ambaye ni Magufuli

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post