Header ads

Header ads
» » Filikunjombe apita bila kupingwa, wapinzani wake waingia mitini

Fomu ya mgombea wa  Chadema ubunge Ludewa zikiwa hazijatimia baada ya tomu ya tamko kukosekana. Fomu ya  mgombea  wa Chadema  ikiwa haijazwa senemu ya  tarehe ,mwezi na mwaka. blogger-image-737464366
Mzee  Kada  wa Chadema  akimpongeza  mbunge wa  Ludewa, Deo Filikunjombe baada ya kupewa  barua ya kupita bila kupingwa.
Mbunge  wa  Ludewa, Deo  Filikunjombe akizungumza na  wanachama  wa CCM na  wananchi wa Ludewa baada ya  kupita  bila  kupingwa. blogger-image--1715103721 Filikunjombe akionyesha barua ya  kupita bila kupingwa.
Msimamizi  wa uchaguzi jimbo la  Ludewa Bw Wiliam Waziri akimpongeza  mbunge  Filikunjombe  baada ya  kumkabidhi barua ya  kupita  bila  kuingwa  ubunge jana. Na Matukiodaima Blog
ALIYEKUWA  mbunge  wa  jimbo la  Ludewa  Deo  Filikunjombe (CCM)  amepita  bila kupingwa baada ya mgombea  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Barthomew Mkinga  kushindwa  kutimiza Masharti na Taratibu za Ujazaji wa Fomu.
Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Ludewa Bw  Wiliam Waziri alisema jana kuwa Mgombea wa Chadema ameshindwa kutimiza taratibu za ujazaji wa fomu hizo hivyo kukosa sifa ya kuwa Mgombea wa Ubunge hivyo  kumkabidhi  barua rasmi Filikunjombe ya kupita  bila kupingwa.
Waziri alisema kwamba Kati ya wagombea wanne waliochukua fomu aliyetimiza taratibu ni Mgombea wa CCM, Bw. Filikunjombe pekee; Kuwa Wagombea wa DP na TLP walishindwa  kabisa kurejesha fomu huku Mgombea wa Chadema akishindwa kujaza fomu vizuri na kushindwa kurejesha Fomu ya Kiapo cha Maadili ya Sheria za Uchaguzi.
Mgombea  huyo wa Chadema  aliyereja  fomu  ya  wadhamini  bila kujaza tarehe , mwezi  wala mwaka ambao uchaguzi  mkuu utafanyika.
Kwa  upande  wake  mgombea  ubunge  wa TLP Bw  Blanka  Haule  alisema  kuwa alishindwa  kurejesha  fomu hizo  kwa wakati kutokana kukosa picha za  kubandika katika  fomu hiyo kutokana na  hali ya mazingira ya  Ludewa  kukowa  eneo la  kupiga picha hizo.
Kwani  alisema picha  ambazo alipiga Njombe alizisahau  Alikoziweka hivyo  kulazimika  kwenda  kupiga  picha nyingine za haraka kwa muda  wa dakika tatu ila cha kushangaza dakika  tatu za kutoka picha hizo  zilionekana kushindwa  kutoka kwa  wakati na kutoka  saa 11 jioni .
“Nilijipanga kugombea ubunge ili kumpokea ubunge Deo Filikunjombe na  kuendeleza  yale  yote  aliyoyafanya jimboni  ila watu  wa  picha  walinikwamisha na  kushindwa kupata  picha kwa  wakati hivyo kwa  sasa  ndio  basi  tena japo ilikuwa ni  Demokrasia lakini kapita  bila  kupingwa  ndio mbunge  wetu:”
Akizungumzia  hatua ya  mgombea  wao wa Chadema  kushindwa kukamilisha  taratibu za ujazaji wa  fomu  hizo Bw Daniel Songo alisema kuwa mgombea  wao hakuwa makini hata  kidogo kwani alikuwa ni mtu ambae hakutulia na muda  mwingi alikuwa akifikiria juu ya wanachama  wanaohama  chama na kuacha kutulia katika kujaza  fomu hizo.
Japo  alisema chama hicho  kimepoteza  umaarufu  kutokana na  mwenendo wa  viongozi wa juu wa chama  hicho  kuendekeza  siasa za ukanda zaidi na kuacha  kutazama uhai wa chama hicho.
Mwenyekiti  wa CCM wilaya ya  Ludewa Stanle Kolimba  alisema kuwa amepokea kwa  furaha kubwa hatua ya  mgombea  wake wa nafasi ya  ubunge kupita  bila kupingwa na kuwa kazi kubwa kwa sasa  kuhakikisha mgombea  urais wa CCM Dr John Magufuli anapata  kura  za  kimbunga  pamoja na  kupigania kata  zote kuona CCM .
Kwa upande wake  Bw  Filikunjombe  akizungumzia hatua hiyo ya kupita Bila kupingwa alisema ameipokea  kwa vizuri sana kwa  alitegemea wapinzani hao wajitokeze  ili aweze kuwaonyesha kazi  kwa  kuhakikisha  wanaangukia  pua katika uchaguzi huo .
Alisema kazi  kubwa ya  maendeleo ambayo ameifanya katika jimbo hilo kwa miaka mitano na imani kubwa ambayo wananchi wa Ludewa wanayo dhidi yake ilikuwani  vigumu kwa wapinzania hao kupata kura Ludewa.
Bw. Filikunjombe  aliwaomba  wananchi wa Ludewa kura  zote  ambazo  walipanga kumpigia yeye  kuzielekeza  kwa mgombea  Urais Dr Magufuli na kwa madiwani wa CCM na  furaha  yake  kuona wapinzani  wanaambulia  patupu katika  wilaya ya  Ludewa.
 

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post