Header ads

Header ads
» » Mwanafunzi amkata mwalimu kwa panga kisa maksi

 Kigali : Msichana anayesomea St André amkata kwa panga mwalimu wake



Msichana anayejulikana kwa jina la Karamaga Elcy anayesomea PCB (Phyisics, Chemistry and Biology) katika kidato cha 6 kwenye shule ya mtakatifu Andrea ( Gs St André) mjini Kigali, amemkata kwa upanga mwalimu wake anayejulikana kama Gasoma Jean Baptiste kutokana na tatizo la alama ( maksi).
Manafunzi huyo, alimkata kwa upanga aliokuja nao kwenye kikapu, ambapo anasoma akienda nje ya bweni.
Uongozi wa St Andre, umetangaza kwamba mwanafunzi huyo alikuwa na hasira kutokana na alama za chemisty hakupewa na mwalimu, mwanafaunzi huyo jumanne wiki hii alikuja shuleni akiwa na mpaga kwenye kikapu.
Karamaga mara baada ya kuingia kwenye maabara , mwanafunzi huyo alimkata kwa upanga kichwani lakini kwa bahati ya mwalimu hakufariki, alipata jeraha , polisi iliwahi kumpeleka hospitalini CHUK , halafu mwanafunzi alipelekwa polisi kuhojiwa kutokana na tukio hilo.
Akiongea kwa njia ya simu , Spt Mbabazi Modeste, msemaji wa Polisi ya taifa mjini Kigali, amekili habari hizo na kusema kuwa bado wanafanya upelelezi .
Padri Lambert Dusingizimana, Kiongozi wa St Andre akiongea na Makuruki naye amekili kwamba habari hizo ni ukweli , amebaini kuwa wameshangazwa na yaliyofanywa na mwalimu. Ameongeza kuwa wanafunzi wametulizwa.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post