Header ads

Header ads
» » AZAM TV na FERWAFA zasaini mkataba wa kitita cha dola bilioni 2,35 za kimarekani

Timu 16 zitashiriki katika daraja la kwanza kwenye ligi kuu ya soka
Shirikisho la soka nchini Rwanda FERWAFA, jumatatu tarehe 24 Augost 2015, limesaini mkataba na Kampuni ya Azam TV kwa kitita cha bilioni 2,35 dola za kimarekani sawa na franga za Rwanda Bilioni moja na Milioni 700 (1.700.000 ) zitakazolipwa kwa kipindi cha miaka mitanu.

Hafla hiyo imefanyika kwenye makao ya Chama cha cha soka cha Rwanda FERWAFA,Remera jijini Kigali.
Mwenyekiti wa FERWAFA Nzamwita Vincent De Gaulle, amesaini mkataba huo kwa niaba ya FERWAFA huku Rhys Torrington akisaini kwa niaba ya Shirika la habari la Azam likiwa na makao yake makuu jijini Dar es Salaam. Vile vile lina tawi lake nchini Rwanda, Kigali.

Katika mkutano na waandishi wa habari, Nzamwita amesema kwamba ligi ya mwakani itazishirikisha timu 16 , kawaida zilikuwa zikishiriki timu 14, club mbili zitajulikana baada ya mkutano mkuu ujao utakaofanyika mjini Huye tarehe 29- 30 Agosti 2015.
Wameazimia kuwa ligi kuu ya soka mwakani itaitwa AZAM Rwanda Premier League,
Nzamwita Vincent De Gaulle, amebaini kuwa AZAM itakuwa ikitoa kila mwaka elfu miatatu hamsini dola za kimarekani sawa na milioni (256, 200, 000 Frw), miaka minne ijayo watakuwa wakitoa dola elfu 500.

Afisa habari katika shirika la AZAM TV Rhys Torrington amewambia waandishi wa habari kwamba hii ni furaha isiyo na kifani kuwa na ushirikiano na shirikisho la soka nchini Rwanda. ‘’Hii ni siku muhimu ya kihistoria katika dimba la Rwanda, tuko tayari kutoa mchango wa maendeleo ya soka nchini Rwanda’’. Amesema.
Aidha bwana Torrington amesema kwamba Azam TV tayari ina kibali cha kutangaza ligi kuu za soka katika jumuiya ya Afrika ya mashariki ikiwa ni pamoja na Tanzania, Kenya , Uganda na Burundi.

AZAM sasa imepewa kibali cha kuonyesha na kutangaza ligi kuu ya soka daraja la kwanza nchini Rwanda kwa njia ya majina (naming rights) na kwa njia ya sanamu (images rights).

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post