WASTAAFU nchini wameanza kunufaika na huduma ya kupokea malipo yao ya
pesheni kupitia huduma ya kifedha iliyoanzishwa na Shirika la Posta.
Mkuu wa Shirika la Posta, Abdi Mchonga alisema kuwa kwa sasa wazee wamepunguziwa usumbufu wa kusafiri umbali mrefu kufuata huduma zao za malipo na hivyo shirika hilo linajivunia kuwa mkombozi wa watu wanaohitaji msaada.
Kupitia matawi ya Posta yaliyopo nchini kote, huduma mbalimbali za kibenki zimekuwa zikitolewa kwa kushirikiana na Shirika la Posta ili kuweza kurahisisha utoaji wa huduma pamoja na kujipatia kipato kwa shirika hilo ili lisiweze kufilisika kutokana na changamoto za utandawazi.
Alisema kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, watu wengi wameacha kuandika barua na hivyo shirika hilo lingeweza kufilisika.
Ili kukabiliana na changamoto hiyo, waliamua kuanzisha huduma ya kibenki kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za kifedha pamoja na kubuni miradi mingine ya kuendeleza shirika hilo.
Alisema kwa kuwa Shirika la Posta lina ofisi zake kila mkoa, imekuwa msaada mkubwa katika kuwarahisishia wananchi kupata huduma ikiwemo ya kibenki na usafirishaji wa mizigo kwa bei nafuu ukilinganisha na wakitumia mashirika mengine kusafirisha mizigo.
Kutokana na watu wengi kuacha mfumo wa kuandika barua, shirika limeanzisha huduma ya kusafirisha mizigo pamoja na barua chache zinazopatikana kupitia mawakala wanaotumia usafiri wa haraka ujulikanao kama ‘City agent mail’ na kumfikia mteja hadi mahali alipo.
Kupitia huduma hiyo, Mchonga alisema imesaidia kupunguza gharama za usafirishaji kwani badala ya kuajiri watu wengi kazi hiyo inafanywa na watu wachache na hivyo kusaidia shirikia kupunguza gharama za uendeshaji.
Aidha alisema shirika hilo kwa kuzingatia kuwa uandishi wa barua ni taaluma na pia ni sanaa, shirika limekuwa likiendesha programu maalumu kwenye shule za msingi ili kuwawezesha wanafunzi kuendeleza sanaa hiyo muhimu.