Header ads

Header ads
» » Rihanna aweka rekodi mpya kwa kuongoza orodha ya ‘‘Most Digital Single Awards’’ Marekani

Rihanna apiga hatua kubwa katika tasnia ya muziki

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Marekani Rihanna, amekuwa wa kwanza kupitisha rekodi milioni 100 za kipekee katika mfumo wa digital na kuongoza orodha ya ‘‘Most Digital Single Awards.’’
Rihanna mwenye umri wa miaka 27 amefanikiwa kuwapiku wasanii wengine ikiwa ni pamoja na Taylor Swift anayemfuata katika nafasi ya pili na Katy Perry anayeshikilia nafasi ya tatu.
Kampuni ya rekodi za muziki hubainisha takwimu hizo kwa kuhesabu jumla ya mauzo pamoja na wasikilizaji mitandaoni nchini Marekani.
Rihanna amekuwa msanii wa kwanza kuvuka kiwango hicho kikubwa na kuweka rekodi mpya katika historia ya muziki.
Rihanna ni msanii mwenye mafanikio aliyewahi kushinda tuzo nane za Grammy , na kuweza kurekodi albamu saba za kipekee kwa jina lake.
Miongoni mwa nyimbo zake kali zinazotamba na kufanya vizuri katika soko la muziki ni kama vile ‘‘We Found Love’’, ‘‘Stay’’ na ‘‘Only Girl (In The World).’’

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post